CCM Blog, Dar es Salaam
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NIHF) limeingia mkataba na NMB Bank, ili kuwarahisishia Wananchi kujiunga na huduma ya Bima ya Afya kwa kulipa fedha kidogo kidogo kupitia mpango wa Dunduliza ambao NIHF imeubuni ambapo mwananchi atakayehitaji ataweza kulipia kupitia benki hiyo kwa njia ya simu ya mkononi.
Kupitia mpango huo wa Dunduliza mwananchi ataweza kulipa kidogo kidogo kwa ajili yake au familia yake au yeyote anahitaji kumlipia kwa kuchagua vifurushi ya Bima ya Afya ambavyo vilivypewa majina ya 'Najali Afya', Wekeza Afya na Timiza Afya,
Akizungumza wakati wa kutiliana saini mkataba huo, Mkurugenzi Mkuu wa NIHF Bernard Konga katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, amesema ili kujiunga na huduma hiyo ya Dunduliza kwa kutumia simu ya mkononi, mwananchi atapiga namba *150*68# halafu yatafuatia maelekezo ya kufanya.
Konga amesema, NIHF imeanzisha huduma hiyo ili kwezesha wananchi wengi zaidi kupata huduma ya bima ya afya kama azma ya Serikali inavyoelekeza.
HABARI KATIKA PICHA👇
Afisa Mkuu Masoko na Huduma za Wateja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Andrew Singu akitoa maneno ya Utangulizi wakati wa hafla hiyoBaadhi ya Maofisa wa Mfuko wa NIHF na NMB Bank wakiwa kwenye hafla hiyo
Mkurugenzi wa Wanachama wa Mfuko wa NIHF Christopher Mapunda akizungumzia faida za huduma aya Dunduliza, wakati wa hafla hiyo
Christopher Mapunda akifafanua zaidi kuhusu huduma hiyo ya Dunduliza
Baadhi ya Maofisa wa Mfuko wa NIHF na NMB Bank wakiwa kwenye hafla hiyo
Baadhi ya Maofisa wa Mfuko wa NIHF, NMB Bank na Waandishi wa habari wakiwa kwenye hafla hiyo.
Baadhi ya Maofisa wa Mfuko wa NIHF na NMB Bank wakiwa kwenye hafla hiyo
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NIHF) Bernard Konga akizungumza wakati wa hafla hiyo
Mtendaji Mkuu wa NMB Bank Ruth Zaipu, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NIHF) Bernard Konga na Mtendaji Mkuu wa NMB Bank Ruth Zaipu, wakibadilishana hati baada ya kusaini mkataba wa NIHF na benki hiyo kuendesha huduma ya Dunduliza ambayo mfuko huo umebuni ili mwana
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NIHF) Bernard Konga na Mtendaji Mkuu wa NMB Bank Ruth Zaipu, wakipongezana baada ya kusaini mkataba wa NIHF na benki hiyo kuendesha huduma ya Dunduliza ambayo mfuko huo umebuni ili mwana
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NIHF) Bernard Konga na Mtendaji Mkuu wa NMB Bank Ruth Zaipu, wakionyesha hati baada ya kusaini mkataba wa NIHF na benki hiyo kuendesha huduma ya Dunduliza ambayo mfuko huo umebuni ili mwana
Post a Comment