Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Mwandamizi Ashura Mzava mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Janeth Mtega imedai kuwa mshtakiwa ametenda kosa hilo kati ya Januari mosi na Februari 26 mwaka 2020 huko katika eneo la Tabata, jijini Dar es Salaam.
Imedaiwa kuwa siku hiyo, mshtakiwa Daud alisambaza picha za ngono akitumia simu yake mkononi aina ya Tecno T301 kupitia akaunti ya Twitter yenye jina la James Michael @James Michae huku akijua kufanya hivyo ni kosa na kinyume cha sheria.
Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na ameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti aliyopewa likiwemo la kuwa na mdhamini mmoja wa kuaminika, ambapo yeye pamoja na mdhamini huyo walitaliwa kusaini bondi ya sh milioni 5.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamlika na kesi hiyo itatajwa Novemba 2 mwaka huu.
Post a Comment