Featured

    Featured Posts

Video & Picha: PROF. MWAMFUPE AZISAKA KURA KWA KUFANYA KAMPENI ZA MLANGO KWA MLANGO MTAA WA ONE WAY DODOMA

Mgombea Udiwani Kata ya Madukani kupitia CCM, Profesa Davis Mwamfupe akimsikiliza fundi ushonaji nguo Mwajabu Jori akitoa kero zinazowakabili wafanyabiashara wa Mtaa wa One Way jijini Dodoma, alipofanya kampeni za mlango kwa mlango katika eneo hilo. Prof. Mwamfupe ni Meya wa Jiji la Dodoma aliyemaliza muda wake.

Baada ya kusikiliza kero zao, Prof. Mwamfupe  aliwaomba ifikapo Oktoba 28, kumpigia kura yeye, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde na Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli ili wasaidiane kuzitafutia ufumbuzi baadhi ya kero hizo.
Mgombea Udiwani Kata ya Madukani kupitia CCM, Profesa Davis Mwamfupe akimsikiliza fundi ushonaji nguo Robert Elfasi akitoa kero zinazowakabili wafanyabiashara wa Mtaa wa One Way jijini Dodoma, ikiwemo suala la kupatiwa mikopo alipofanya kampeni za mlango kwa mlango katika eneo hilo. Aliyesimama kushoto ni Katibu wa CCM Kata ya Madukani, Yahaya Mwingi.
Mwamfupe akiwa na  baadhi ya viongozi wa CCM Kata ya Madukani yalipo Makao Makuu ya CCM. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo. Jamila Ashery.
Mwamfupe akiwa ameongozana na  baadhi ya viongozi wa CCM Kata ya Madukani. Katikati ni  Katibu UWT CCM wa kata hiyo, Amina Mohamed. 

Mwamfupe akiwa na Katibu wa CCM Kata ya Madukani wakiondoka baada ya kumaliza kampeni za Mlango kwa Mlango katika Mtaa wa Madukani katikati ya Jiji la Dodoma.
Mwamfupe akizungumza na mmoja wa wafanyabiashara wa mtaa huo.

PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
0754264203
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana