Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Kuwait hapa nchini amemkabidhi Balozi wa Kuwait Mhe.Mubarak Mohammed Alsehaijan barua iliyoandikwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenda kwa Kiongozi mpya wa Kuwait.
Prof. Kabudi amesema Tanzania na Kuwait zina mahusiano mazuri sana na muda mrefu katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo akitolea mfano wa mfuko wa Kuwait ambao umekuwa wa msaada mkubwa katika kwa Tanzania ambao umekuwa ukisaidia katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali hapa nchini ikiwemo barabara.
Ameongeza kuwa msiba wa Kiongozi huyo wa Kuwait ni msiba wa Watanzania wote kwa kuwa kwa muda wote ambao Hayati Sheikh Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-sabah amekuwa Kiongozi wa Taifa hilo amekuwa karibu sana na Tanzania.
Post a Comment