CCM Blog, Dar es Salaam
Rais wa Sita wa Malawi Dk. Larus McCarthy Chakwera kesho atawaili nchini kwa ajili ya ziara ya Kitaifa ya siku tatu kwa mwaliko ya Rais Dk. John Magufuli ambaye ndiye atakayempokea huyo kesho mgeni huyo atakapowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Profesa Palamagamba Kabudi amesema leo kwamba ziara hiyo ni ya kwanza tangu aingie madarakani Juni mwaka huu na ziara nyingine alizokwishafanya ni siku moja moja katika nchi za Zambia na Zimbabwe.
Amesema lengo la ziara yake hapa nchini ni kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Malawi na kuendeleza kudumisha ujirani mwema.
Ziara hiyo imekuja huku Rais Dk. Magufuli akiwa tayari alishafanya ziara ya siku mbili nchini Malawi ziara ambayo aliifanya kuanzia Aprili 24 mwaka jana huku Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan naye alikwenda nchini Malawi Julai 6, mwaka huu na kushiriki sherehe za uzinduzi rasmi wa serikali ya Rais wa nchi hiyo Dk. Larus.
Profesa Kabudi amesema Mgeni huyo atatembelea Bandari ya Dar es Salaam, ambako ataona shughuli mbalimbali zinavyofanyika katika bandari hiyo na uboreshwaji wa miundombinu unaoendelea na pia atakagua Kituo cha kuhifadhi mizigo ya malawi.
Pia Rais huyo wa Malawi akiwa na mwenyeji wake Rais Dk. John Magufuli ataweka jiwe la msingi la Kituo kipya cha kisasa cha mabasi ya kwenda mikoani kilichopo Mbezi mwisho, wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam.
Post a Comment