Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewaonya viongozi wa vyama vya siasa nchini wanaoingiza vijana kwenye mambo ya uhalifu kuendelea kupambana na siasa na si uhalifu.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam, IGP Sirro, amesema kuwa uhalifu hauwezi kuwafanya wao kuwa viongozi huku akidai kuwa uwepo wa baadhi ya wananchi wachache walioandaliwa kufanya vurugu.
“Niwaombe sana wanasiasa pambaneni na mambo ya siasa msijaribu kuingiza vijana kwenye mambo ya uhalifu, uhalifu hauwezi kukufanya ukawa kiongozi sanasana mnawaharibia vijana maisha yao, maarifa yao, mwisho wa siku wanapata adhabu wanafungwa wanaacha familia zao” IGP Sirro
“ Niwaombe sana pambaneni na siasa muweze kuwa viongozi lakini msitiumie vijana kuwaingiza kwenye uhalifu wakipata shida na familia zao wakati nyinyi mnaenjoy maisha na familia zenu” IGP Sirro.
Post a Comment