Na Allawi Kaboyo- Bukoba.
Zikiwa zimebaki siku chache kuelekea Uchaguzi Mkuu ufanyike Oktoba 28 mwaka huu, Wananchi wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wameaswa kutofanya makosa katika Uchaguzi huo kwa kuwachagua viongozi ambao hawataweza kuwaletea maendeleo na kubaki wanajilaumu.
Hayo yamesemwa na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani hapa, wakati wa mkutano wa kampeini za CCM uliofanyika katika Kata ya Kashai ambapo viongozi hao wameeleza kuwa tayari wananchi wa Bukoba mjini wameshaonja joto baya la kutawaliwa na upinzani hivyo hawana sababu ya kuchagua upinzani tena.
Akiongea katika jukwaa hilo aliyekuwa katibu mwenezi wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa Evance Kamenge amesema kuwa vyama vya upinzani kwa sasa havina sera na badala yake vibakia na viroja ambavyo haviwezi kuwaletea maendeleo Watanzania.
Kamenge amesema kuwa miaka mitano iliyopita Rais Dk. John Magufuli ameweza kutekeleza mambo yote yaliyokuwa yakipigiwa kelele na wapinzani na sasa wamebaki wameduwaa hawana sera.
“Mimi nilikuwa upinzani na niliwahi kugombea ubunge nukiwa upinani mwaka 2015, baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani sera tulizokuwa tukizipigia kelele amezitekeleza tena kwa kiwango ambacho na sisi tusingeliweza, kutokea hapo nikaona mimi kama kija mzalendo sina sababu tena ya kuendelea kuwa upinzani ndo maana mnaniona hapa nikikitafutia kura za kishindo chama cha mapinduzi.” Amesema Kamenge.
Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa mkoa wa Kagera Hamimu Mahamudu amewakumbusha wananchi wa Manispaa ya Bukoba pamoja na Kata Kashai kuwa kwa miaka mitano wakuwa wakitawaliwa na upinzani ambapo kwa miaka hiyo wamejionea hali ilivyokuwa ikiwemo kuzorota kwa maendeleo katika maeneo yao huku waliowachagua wakiwa wamewakimbia.
Ameongeza kuwa pamoja na mambo ambayo chama hicho kimefanya bado kwa Bukoba mjini kutokana na kuwepo kwa upinzani limeshindwa kujengwa soko la kisasa pamoja na kiuo cha mabasi cha kisasa na badala yake halmashauri iliyokuwa ikiongozwa na upinzani imekuwa ikitoa huduma kwa kubagua.
Aidha Mahamudu amesema kuwa katika kipindi hiki cha kampeini wananchama wao wamekuwa wakitishiwa maisha kwa kutolewa vitisho mbalimbali endapo wataichagua CCM, ambapo ametumia fursa hiyo kuwasihi wanachama wake kuwa watulivu na wasiwe na woga wajitokeze kupiga kura na kuwachagua wagombea wa CCM.
“Tunazo taarifa kuwa mnatishwa hasa nyie akina mama, tumesikia kwenye majukwa baadhi ya wagombea wakitishia kumwaga damu endapo hawatachaguliwa, mimi niseme tu mara hii tumeamua liwe jua iwe mvua CCM ushindi ni suaa la lazima, na wanaotishia kumwaga damu wamwage tu hata mkojo watakiona chamtemakuni.” Amesisitiza Hamimu.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Constatia Buhiye mkoa wa Kagera akiongea kabla ya kumkabidhi ilani ya uchaguzi mgombea wa udiwaniwa kata ya Kashai alisema kuwa jimbo la Bukoba wananchhi wake wamekuwa yatima kwa kipindi kirefu sana hivyo wanapaswa kufanya maamuzi sahihi kuhakikisha chama chao kinashinda kwenye uchaguzi mkuu.
Buhiye amesema kuwa kwa sasa wananchi wanatakiwa wafanye maamuzi ya uelewa na sio kupiga kura za ushabiki ili kuhakikisha wanaleta maendeleo katika maeneo yote ya mkoa wa Kagera ambapo amewaomba wananchi kumchagua mgombea ubunge wa jimbo la Bukoba Stivene Byabato na kura nyingi kwa Rais Magufuli pamoja na madiwani wote wa CCM ili kupitia wao watapata wabunge wanne waa viti maalumu kutoka Kagera.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera Constansia Buhiye akikabithi Ilani ya CCM ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025 kwa Mgombea Udiwani Kata Kashai Ramadhani Kambuga katika Mkutano wa Kampeini za CCM uliofanyika kata Kashi mtaa wa Katatolanso. Baadhi ya wananchi wa waiojitokeza kwenye mkutano wa kampeini za CCM Kata Kashai kusikiliza sera zinazotolewa na viongozi pamoja na wagombea wa chama hicho.
Post a Comment