Featured

    Featured Posts

WANANCHI KAGERA WASHAURIWA KUFANYA MAZOEI ILI KUJIKINGA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA

Na Allawi Kaboyo – Bukoba.

Kutokana na kushamili kwa magonjwa yanayoitesa jamii hasa magonjwa ya kisukari, Presha, kuongezeka uuzito usiokuwa na mpangilio, mkuu wa mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amewataka wanakagera kujikita katika kufanya mazoezi ya viungo ili kujiepusha na matatizo hayo.


Gaguti  ametoa ushauri huo  wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo kipya cha mazoezi (GYM) Okitoba 09,mwaka huu kinachomilikiwa na kampuni ya TRS kilichopo manispaa ya Bukoba.


Katika hotuba yake Mkuu wa Mkoa amewataka wanankagera kuwa wanatakiwa kujijengwa mazoea ya kufanya mazoezi ili kuhimarisha afya zao na kuweza kujiepusha na maradhi yanayowasumbua wananchi wengi.


Amesema kuwa uwepo wa kituo hicho kitakuwa moja ya kichocheo cha maendeleo katika mkoa wa Kagera kutokana na Mkoa huo kupakana na nchi takribani 4 za Afrika Mashariki, hivyo wageni watakapokuwa wanaingia hapa nchini watapata sehemu sahihi ya kufanyia mazoezi na kutuingizia pesa za kigeni.


“Niwapongeze sana wawekezaji waliobuni mradi huu, kusema kweli katika mkoa wa Kagera kituo hiki ndicho kituo bora sijapata kuona tangu niingie Kagera. Niwaoombe wanakagera wenzangu tukitumie kufanya mazoezi kwaajili ya kuhimarisha afya zetu, mimi ni  mdau  mkubwa wa mazoezi na nitakuwa nakuja hapa kufanya mazoezi.” Amesema Gaguti.


Aidha ameongeza kuwa pamoja na uwepo wa kituo hicho cha mazoezi pia watanzania na wageni watapa fursa ya kunywa kahawa ya TANICA inayozalisha mkoani humo na inayolimwa Kagera na kupelekea kuitangaza kahawa hiyo kitaifa na kimataifa huku akibainisha faida mbalimbali za unywaji wa kahawa.


Kwaupande wake mkurugenzi wa kituo hicho Evance Kamenge amesema kuwa uwepo  wa kituo hicho basi uwe sababu ya kupunguza magonjwa yasiyalazima kwa wanankagera  kwa kuwa kituoni hapo wapo  wataalamu wa afya pamoja na mazoezi sahihi ya mwili.


Kamenge amesema kuwa wadau wote watakaofanya mazoezi katika kituo hicho wataweza kupewa ushauri na madaktari wabobezi wa viongo na kuweza kufanyishwa mazoezi sahihi na kwa wakati sahihi.


Msanii maarufu wa muziki wa taarabu maarufu kama mzee Yusuph amefika katika kitu hicho na kuupongeza uwekezaji uliwekwa pale na kusema kuwa kituo hicho kimekuwa kituo bora na kuwataka wanakagera kukitumia kufanya mazoezi.


Mmoja wa walimu katika kituo hicha amesema kuwa katika kipindi hiki amegundua jamii ya wanakagera na Bukoba kwaujumla wanasumbuliwa na matatizo ya ulaji wa vyakula sahihi suala linalowapekelea uwa na matatizo ya kuwa na vitambi pamoja na kuwa na uzito mkubwa.

Mkuu wa mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti akiwa kwenye moja ya mashine ya kufanyia mwili masaji katika kituo cha  TRS health CLUB baada ya kukizindua mjini Bukoba.
Msanii maarufu kutoka jijini mwanza aliyejulikana kwa jina la Dkt. Bahati akitoa burudani kwa wananchi waliojitokeza kwenye hafla ya uzinduzi wa kituo cha mazoezi TRS health CLUB Bukoba.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana