Featured

    Featured Posts

KIKWETE AHUDHURIA HARUSI YA HAJI MANARA, ASEMA NDOA HAINA UFUNDI ZAIDI YA WENZA KUSTAHMILIANA





Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara, usiku wa kuamkia jana Desemba 10, alifunga ndoa na mkewe Naheeda, katika msikiti wa Masjid Maamur, jijini Dar es Salaam.


Ndoa yake imehudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dk. Jakaya Kikwete, Shehe Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum na watu wengine wengi maarufu.


Kikwete amesema kuwa Haji alimfuata nyumbani na kumshirikisha jambo hilo kwa ajili ya ndoa na akamuahidi kuja.


"Hakuna ufundi kwenye ndoa,  kikubwa ni kustahimiliana na kuvumiliana.


Mnapaswa kuwa makini na kusikilizana katika ndoa, pia nakushauri kwamba uwe na uvumilivu na kuona namna gani mnaweza kuleta watoto kwa kuulizana na kujua mambo yatakuaje." Amesema Kikwete akimpa wosia Haji Manara.


"Baraka za Mungu kwa watoto ni zake ka kadri atakavyoamua, yale makundi yaache kwa kuwa kila mmoja anajua anachokipenda.


Nilikuwa ninazungumza na mzee hapo nyuma akaniambia kwamba anahitaji wajukuu hivyo ni jambo la kheri na linahitaji subira kikubwa ninawapongeza katika hilo na ninaamini kwamba itakuwa kheri," amesema.


author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana