Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB – Ruth Zaipuna, alipokuwa akielezea namna Benki ya NMB imejipanga kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kukuza uchumi na kuisaidia jamii, alipowasili katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar. Waliongozana na Bi. Ruth ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara Benki ya NMB – Filbert Mponzi(kati) na Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa Benki ya NMB – Alfred Shao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Kadi yake ya NMB Mastacard World Debit na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB – Ruth Zaipuna, baada ya kumaliza mazungumzo yao katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB – Ruth Zaipuna, alipowasili katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar kwa ajili ya mazungumzo na kumpongeza akiwa na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara Benki ya NMB – Filbert Mponzi(kati), Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa Benki ya NMB – Alfred Shao na Mkuu wa Biashara Zanzibar wa Benki ya NMB – Abdalla Duchi.
Post a Comment