Featured

    Featured Posts

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE DESEMBA 15, 2020

 

Gareth Bale

Winga wa Wales Gareth Bale, 31, inatarajia kufanya vyema Real Madrid msimu huu baada ya kuwa Tottenham kwa mkopo. (AS)

Southampton wanapania kumsajili kwa mkopo mchezaji wa safu ya kushoto na nyuma wa Manchester United Muingereza Brandon Williams, mwezi Januari. (Telegraph)

West Ham inaweza kumsajili kiungo wa kati wa Lyon Mrazil Marcelo, 33, kwa mkataba wa bure msimu ujao. (Sun)

West Ham inaweza kumsajili kiungo wa kati wa Lyon Mrazil Marcelo(Kulia)
Maelezo ya picha,

West Ham inaweza kumsajili kiungo wa kati wa Lyon Mrazil Marcelo(Kulia)

Kiungo wa kati wa Inter Milan Christian Eriksen, 28, hana mpango wa kurudi katika Ligi ya Primia na hajakubali kuhamia Paris St-Germain. (Star)

Mlinzi wa Arsenal mfaransa William Saliba, 19, yuko tayari kucheza kwingine kokote England kwa mkopo badala ya kurejea Ufaransa mwezi Januari. (The Athletic - subscription only)

Rais wa Juventus Andrea Agnelli amesema klabu hiyo imempatia ofa ya kurefusha mkataba mshambuliaji Muargentina Paulo Dybala, baada ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27- kudai hajapewa mkataba wowote. (Tuttosport via Football Italia)

Paulo Dybala

Mshambuliaji wa Watford Troy Deeney anasema mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta lazima afanye mkutano wa dharura na wachezaji baada ya klabu hiyo kushindwa na Burnley wikendi iliyopita. (Talksport)

Everton ina imani ya kusalia na mchezaji wa safu ya kushoto na nyuma Muingereza Thierry Small licha ya mchezaji huyo aliye na umri wa miaka 16 kunyatiwa na Arsenal, Bayern Munich na Juventus. (Liverpool Echo)

Mikel Arteta
Maelezo ya picha,

Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta ahauriwa kufanya mkutano wa dharura na wachezaji

Mshambuliaji wa zamani wa Leeds Noel Whelan anasema winga Mreno wa klabu hiyo Helder Costa "hakusaidia kwa lolote" ikatika kipindi cha pili cha mechi yao dhidi ya West Ham ambapo walishindwa mabao 2-1. (Football Insider)

Tetesi za Soka Jumatatu

Kiungo wa kati wa Juventus Mjerumani Sami Khedira, 33, ambaye anapanga kuhama klabu hiyo mwezi Januari, amethibitisha kuwasiliana na mkufunzi wa Everton Carlo Ancelotti. (Bild - in German)

Sami Khedira
Maelezo ya picha,

Sami Khedira athibitisha kuzungumza na Everton

Everton wako tayari kumpatia ofa ya uhamisho wa bila malipo kiongo wao wa kati Dele Alli, 24 mwezi Januari kwa lengo la kuikosesha Tottenham Hotspur nafasi ya kumsajili. (Star)

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema kuwa kiongo wa kati Mhispania Isco hayuko katika mipango yake ya siku zijazo. Hata hivyo, kiungo huyo aliye na umri wa miaka 28-anatarajiwa kuondaka klabu hiyo mwezi Januari. (Marca - in Spanish)

Isco

Paris St-Germain huenda ikamsajili mshambuliaji wa Lyon Mholanzi Memphis Depay msimu ujao lakini Barcelona wamekuwa wakimnyatia kwa muda mrefu kiongo huyo aliye na umri wa miaka 26. (Le Parisien - in French)

Tottenham wako tayari kulipa Juventus £63.6m kumunua mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 27. (TodoFichajes - in Spanish)

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana