Bao la Southampton lilikuwa ni la kujifungwa la mlinzi wa Arsenal , Gabriel ambaye alijikuta aukiuweka kimiani mpira wa krosi uliopigwa na Kyle Walker Peters dakika ya 24 ya mchezo.
Lilikuwa ni bao la kwanza kwa Arsenal kuruhusu baada ya dakika 508 na pia kilikuwa kipigo cha kwanza kwa The Gunners baada ya michezo takribani 7 kucheza bila kupoteza.
Arsenal ilikosa huduma ya mshambuliaji wake Pierre Emerick-Aubameyang na Emile Smith Rowe lakini ilimtumia Bukayo Saka katika kipindi cha pili cha mchezo huo
Akizungumzia kipigo hich, kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amesema ni bahati mbaya sana wameondolewa katika michuano hiyo kwakuwa walikuwa na matatizo ya kiufundi uwanjani hususan kipindi cha kwanza cha mchezo.
Ni kwa mara ya kwanza Southampton inaitoa timu bingwa katika mashindano tangu wafanye hivyo mwaka 1902 walipoinyuka Tottenham Hotspurs, lakini pia ni kwa mara ya kwanza ndani ya misimu minne iliyopita, Arsenal wanaondolewa katika mashindano hayo.
Post a Comment