Tangazo la Tanzia lililotolewa mchana huu na Spika wa Bunge Job Ndugai limesema kifo cha Mbunge huyo kimetokea leo Januari 21, 2021 saa 7 usiku (kwa saa za India) akiwa katika Hospitali ya HCG Mumbai, India alikokuwa anapatiwa matibabu.
“Nimepokea kwa mstuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe. Martha Umbulla. Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, Waheshimiwa Wabunge na wananchi wa Mkoa wa Manyara. Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Spika Ndugai.
Post a Comment