Featured

    Featured Posts

MJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM RAIS DK. HUSSEIN MWINYI AZUNGUMZA VIONGOZI WA CCM WILAYA YA KATI, UNGUJA, ATOA SHUKRANI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Viongozi wa CCM na Mabalozi wa Mashina wa CCM wa Wilaya ya Kati, Unguja akiwa katika ziara yake ya kutoa shukrani. Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein, Tunguu (SUZA) Wilaya ya Kati Unguja jijini Zanzibar. Pamoja na mambo mengine Dk. Mwinyi ametumia fursa hiyo kutoa shukrani kwa viongozi hao kusimama imara na kuiwezesha CCM kushinda kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu uliopita ikiwemo yeye kushinda Kiti cha Urais.
 
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Mabodi akizungumza wakati wa mkutano. Kushoto ni  Mke wa Rais Mama Mariam Mwinyi


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk. Hussein Ali Mwinyi akifuatilia Taarifa ya Wilaya ya Kati Unguja ikiwasilishwa , wakati wa mkutano wake wa kutoa shukrani kwa Mabalozi wa CCM wa Wilaya ya Kati Unguja uliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu (SUZA) kutoka kulia ni  Mke wa Rais Mama Mariam Mwinyi   akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Mabodi. 


VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kati Unguja wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza kwenye mkutano huo


BAADHI ya Mabalozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kati Unguja wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk. Hussein Ali Mwinyi


VIONGOZI wa CCM wa Wilaya ya Kati na Mabalozi wa Mashina wa CCM wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk.Hussein Ali Mwinyi.


MABALOZI wa Mashina wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kati Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk. Hussein Ali Mwinyi.(Picha zote na Ikulu, Zanzibar)
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana