Featured

    Featured Posts

RAIS DK. MAGUFULI AOMBOLEZA KIFO CHA MBUNGE MARTHA UMBULLA, ASEMA ANAKUMBUKA ALIVYOKUWA MCHAPAKAZI TANGU AKIWA DC

 Rais Dk. John Magufuli

Rais Dk. John Magufuli amesema amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Martha Jachi Umbulla aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Manyara kilichotokea leo tarehe Januari 21, 2021  Mumbai nchini India alikokwenda kwa ajili ya kupatiwa matibabu.


Kufuatia kifo hicho Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge Job Ndugai, familia ya Marehemu Martha Umbulla, Wabunge wote, wananchi wa Mkoa wa Manyara na wote walioguswa na kifo hicho.


“Martha Umbulla alikuwa mpole, mchapakazi na mpenda maendeleo. Nazikumbuka jitihada zake za uongozi akiwa Mkuu wa Wilaya na akiwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” amesema Rais Magufuli akikaririwa katika taarifa iliyotolewa na Ikulu.


Taarifa hiyo imesema Rais amewaomba wanafamilia wote wawe na moyo wa uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi kigumu cha majonzi na amemuombea Marehemu Martha Jachi Umbulla apumzike mahali pema peponi, Amina.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana