Featured

    Featured Posts

MALAWI WAJA TANZANIA KUJIFUNZA NAMNA YA KURATIBU NA KUSIMAMIA ASASI ZA KIRAIA (NGOs)

 


Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Kundi la Asasi za
Kiraia (NGOs) Mh.Neema Lugangira akizungumza wakati wa ziara hiyo


Waziri wa Jinsia,Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Malawi,Patricia Kaliati katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto wa Tanzania anayshughulikia Maendeleo ya
Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Dkt John Jingu kulia na  Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Kundi la Asasi za
Kiraia (NGOs) Mh.Neema Lugangira kushoto

Msajili wa NGOS wa kwanza kulia akifuatilia matukio mbalimbali wakati wa ziara hiyo.


TANZANIA imepata ugeni mkubwa kutoka nchini Malawi ambao wamekuja mkoani Dodoma nchini Tanzania kujifunza namna ya kuendesha masuala ya Asasi za Kiraia (NGOs).

Akizungumza wakati wa ziara ya ugeni,Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Mh.Neema Lugangira alisema ugeni huo umekuja Tanzania kujifunza na umegongozwa na  Waziri wa Malawi anayesimamia Masuala ya Jinsia ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii.

Alisema Waziri huyo ameongozana na Katibu Mkuu wa Ziara ya Afya na Mwenyekit wa Kamati ya kudumu ya Bunge ambayo inasimamia masuala ya Jinsia Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii .

Wakiwemo Mbunge ambaye ni Mjumbe wa Kamati hiyo na Bodi ya NGOs ambayo inajukumu la kuratibu shughuli zote za NGOs nchini Malawi na upande wa Tanzania uliongozwa Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii ,Msajili wa NGos Tanzania na Mwenyekiti wa Bodi ya NGOs Tanzania  na yeye kama Mbunge wa NGOs.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mbunge Neema alisema lengo la ugeni huo wenzao wa Malawi wapo kwenye mchakato wa kwenda kufanyia maboresho sheria yao ya NGOs hivyo wamejaribu kuangalia kwenye nchini za Afrika ambazo zimefanya vizuri kuratibu na kusimamia shughuli za NGos ili kuhakikisha shughuli hizo zinapelekea maendeleo ya wananchi.

Alisema wananchi hao ni wale ambao wapo kwenye ngazi ya jamii walivyoratibu wakaona Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo zimefanya vizuri na mapinduzi makubwa kwenye eneo hilo kuhakikisha shughuli za NGos zinasimamiwa ipaswa na zinaendana sambamba na malengo ya Taifa na shughuli hizo zinawanufaisha wananchi wanyonge wa Tanzania.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto wa Tanzania anayshughulikia Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Dkt John Jingu alisema lengo la ziara yao ni kujifunza kuona namna gani nzuri wao wanavyofanya katika kuratibu shughuli za mashiriki yasiyo ya kiserikali.

Alisema jambo kubwa nzuri ambalo wamefurahia ni namna gani ambavyo mashirika hayo yanavyofanya kazi kwa kushirikiana na serikali na namna walivyoweka misingi ya uwazi na uwajibika kwenye shughuli za mashirika.

Alisema wamejifunza uzoefu wa kwao na kuna mambo wanafanya yanafafana nasi lakini jambo moja wote tunathamini mchango wa mashirki yasiyo ya kiserikali unatoa kwenye maeneo ya nchi wote.

Hata hivyo alisema kwamba wanaona kuna umuhimu wa kuona mashirika hayo yafanye kazi kwa uwazi na uwajibikaji lakini kwa kushiriki wananchi ili mchango wao uwezo kufanikika kwenye maeneo ya nchi

Naye kwa upande wake akizungumza wakati wa ziara hiyo, Waziri wa Jinsia,Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Malawi,Patricia Kaliati akizungumza wakati wa ziara hiyoalisema wamekuja Tanzania kuangalia maendeleo walionayo na kuona  namna wanavyozingatia sheria mbalimbali za NGOs.

Alisema wakati wanakwenda kwenye Bunge na wataweza kufanya kazi kwa kushirikiana na NGos kwa kuzingatia sera ya serikali inavyotaka ili kuhakikisha zinakuwa chachu kubwa katika kupata mafanikio.

Hata hivyo Mbunge kutoka nchini Malawi Saveoipo Kafafa alisema wamekuja kuzungumza na serikali ya Tanzania na wabunge wa Tanzania kwa ajili ya maendeleo ya NGos hapa Tanzania.

Alisema nchini mwao Malawi wanafanya maboresho ya katiba ya maendeleo ya NGOs kwenye bunge na wameendelea vizuri na mambo mengi mazuri ambayo yatakuwa chachu kuweza kupata mafanikio .

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana