Vingunguti, Dar es Salaam
Uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Mtambani Kata ya Vingunguti chini ya Mwenyekiti wake Omary Kabatele umewasilisha taarifa ya kazi kwa Wananchi wa Mtambani mbele ya Meya ya Manispaa ya Ilala Diwani wa Kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto.
Akizungumza baada ya kuwasilishwa taarifa hiyo, Meya Kumbilamoto ametoa shukrani kwa Wananchi wa Mtaa wa Mtambani kwa kukichagua cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 huku akimuagiza Mtendaji wa Kata hiyo ya Vingunguti kuitisha kikao siku ya Jumatano katika Ofisi yake, baada ya kujitokeza changamoto ya maji katika mkutano huo.
Meya Kumbilamoto amesema lengo la kikao hicho ni kuwaelekeza Jumuia ya watumia maji wa Mtambani watoke kwenye utiaji wa saini katika Akaunti ya benki kwa kuwa Mradi wa maji uliopo kwa sasa umehama kutoka Halmashauri kwenda Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoa wa Dar es Salaam (Dawasa) na Akaunti hiyo inakuwa chini ya Mtendaji Kata.
Amesema kikao hicho kitawakutanisha watu wa Dawasa, jumuia ya watumia maji Mtambani pamoja na watia saini kwenye Akaunti ya watumia maji Mtambani na kwamba Dawasa wanashindwa kutoa fedha kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za maji kutokana na watia saini kutoka katika jumuia ya watumia maji kutokubali kutoka katika kutia saini kwenye maswala ya Kibenki.
Meya wa Manaispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza na Wananchi, aliposhiriki mkutano wa wananchi wa Mtaa wa Mtambani Kata ya Vingunguti, leo.Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Mtambani, wakimsikiliza Meya wa Manaispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto alipokuwa akizungumza aliposhiriki mkutano wa wananchi katika huo katika Kata ya Vingunguti, leo. (Habari na Picha kwa Hisani ya Meya Kumbilamoto).
Post a Comment