Featured

    Featured Posts

NDEJEMBI ATAKA KILA MTUMISHI WA UMMA KUWA NA MPANGO KAZI ILI KUONDOKANA NA UFANYAJI KAZI WA MAZOEA

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi akizungumza na Watumishi wa Umma, Wilayani Mpwapwa wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kutatua changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma na kuhimiza uwajibikaji na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini. Picha zaidi chini ya stori

James Mwanamyoto, Mpwapwa

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi amemtaka kila Mtumishi wa Umma nchini kuwa na mpango kazi utakaomuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi na kutoa huduma bora kwa umma.


Ndejembi ametoa maelekezo hayo jana, Februari 17, 2021, wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani Mpwapwa na Kongwa mkoani Dodoma na kusema ni jukumu la Waajiri kuhakikisha kila mtumishi anatekeleza mpango kazi wake ili kutoa mchango wa kiutendaji mahala pa kazi badala ya kuendelea kufanya kazi kwa mazoea jambo ambalo halina tija katika maendeleo ya taifa.


Ndejembi amewasisitiza pia Watumishi wa Umma kuzingatia ujazaji wa fomu za Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) ili kutoa fursa kwa Waajiri kupima utendaji kazi wa watumishi wao kwa lengo la kuwapa stahiki kulingana na utendaji kazi wao.


“OPRAS ipo kwa mujibu wa Sera ya Menejimenti na Ajira ya Mwaka 1998 kama ilivyorekebishwa Mwaka 2008 pamoja na Sheria ya Utumishi Sura Namba 298, hivyo ni jukumu la waajiri kuhakikisha watumishi wanajaza fomu na kufanyiwa tathmini ya utendaji kazi wao ili kuongeza ufanisi kiutendaji,” Ndejembi amesisitiza.


Akijibu hoja ya Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Kandindo Mumeli, kuhusu baadhi ya waajiri kutotenga bajeti ya kuwahudumia Watumishi wa Umma wenye Ulemavu kama Mwongozo wa Huduma kwa Watumishi wa Umma wenye Ulemavu wa Mwaka 2008 unavyoelekeza, Ndejembi amewataka Waajiri kutoa kipaumbele cha kutenga fedha za kuwahudumia watumishi hao ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kikamilifu.


Aidha, Ndejembi amesisitiza juu ya usimamizi wa ruzuku inayotolewa na Serikali kwa wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, ambapo amesema, ni jukumu la kila Mtumishi wa Umma kuhakikisha fedha wanazopokea wanufaika wa TASAF zinatumika kuboresha maisha yao kwa kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo.


“Kumekuwa na mtazamo hasi juu ya usimamizi wa fedha za TASAF kuwa ni jukumu la Waratibu wa TASAF pekee, jambo ambalo halina tija kwa taifa kwani usimamizi wa fedha za umma ni jukumu la kila mtumishi, hivyo ni wajibu wetu sote kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa,” Ndejembi ameongeza.


Pia, Ndejembi amepiga marufuku kitendo cha kukata fedha za wanufaika wa TASAF ili kuchangia Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwani kitendo hicho kinawakwamisha wanufaika kutumia ruzuku waliyopewa katika shughuli mbalimbali za maendeleo zitakazoboresha maisha yao.


Ndejembi ameongeza kuwa, wanufaika wa TASAF waachwe huru kutumia ruzuku wanazopatiwa katika shughuli mbalimbaliz za maendeleo ili watakachozalisha ndio wakitumie kuchangia CHF kwa hiari.


Lengo la ziara ya Ndejembi katika Wilaya hizo ilikuwa ni kutatua changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma na kuhimiza uwajibikaji na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.

Picha zaidi👇


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo wakati akizungumza na Watumishi wa Umma, Wilayani Mpwapwa wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kutatua changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma na kuhimiza uwajibikaji na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kutatua changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma na kuhimiza uwajibikaji na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kutatua changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma na kuhimiza uwajibikaji na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini
Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Kandido Mumeli Akiwasilisha hoja ya kiutumishi kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la kutatua changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma na kuhimiza uwajibikaji na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini. (Picha zote na Mapigapicha Maalum)

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana