CAG Kichere ameyabainisha hayo leo Machi 28, 2021 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma wakati akiwasilisha Ripoti ya Ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
"Katika ukaguzi wetu wa mwaka 2019/2020 tumegundua Shirika letu la Ndege limetengeneza hasara mwaka huu ya Tsh.Bilioni 60 ila kwa miaka mitano pia limekuwa likitengeneza hasara, kuna changamoto ambazo Sarikali inabidi iziangalie ili Shirika letu litekeleze majukumu yake vizuri,"amesema.
Pia amesema kuwa, "Miradi ambayo nimefanya ukaguzi ni Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka DSM hadi Makutupora, mradi wa ujenzi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP), mradi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka kwa DSM (UDART) Gerezani mpaka Mbagala.
"Mradi wa upanuzi wa barabara ya Morogoro kutoka Kimara hadi Kibaha, mradi wa usambazaji maji wa Same, Mwanga na Korogwe, na mradi wa uzalishaji sukari huko Morogoro,"amesema CAG Kichere.
Post a Comment