Hombolo, Dodoma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Isdor Mpango amelishukuru Shirika la Teresia wa Mtoto Yesu lenye Makao Makuu yake Nchini india kwa kazi nzuri wanayoifanya kuisaidia Tanzania katika kazi ya kuwatunza Watoto Yatima, Wazee na wenye Mahitaji maalum.
Makamu wa Rais Dk. Mpango ametoa shukrani hizo akizungumza alipotembelea katika Kituo cha kuwatunza Watoto yatima, Wazee na wenye Mahitaji Maalum cha Huruma Missionary Sisters of charity kiliopo Hombolo jijini Dodoma, leo kwa lengo la kuwapatia faraja watoto na wazee hao.
Amesema ataimiza Wizaya ya Afya na Maendeleo ya Jamii kitengo cha Ustawi wa Jamii wafike katika Kituo hicho ili waweze kufanya kazi ya kutoa huduma zaidi. Kituo hicho kinachotunza Watoto Yatima, Wazee na wenye Mahitaji Maalum kina jumla ya watu 90 wenye uhitaji wa aina mbalimbali.
Makamu wa Rais Dk. Mpango kwenye kituo hicho ametoa vifaa mbalimbali ikiwemo vyakula, Sabuni, Vinywaji na fedha taslim Sh. Milioni 5 kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka, ambapo pia amewasilisha salam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuwatakia Watanzania wote heri ya Sikukuu ya Pasaka na kuendelea kufanya kazi ili kuweza kuijenga nchi ya Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Isdor Mpango, akikabidhi Vifaa mbalimbali na fedha taslimu Sh. Milioni 5 kwa Sister Prodencia wa Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Watoto wa Yesu Kanisa Katoliki Jimbo Kuu Nzinje Dodoma, kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka kwa Watoto Yatima, Wazee na Watu wenye Mahitaji Maalum wanaotunzwa katika Kituo cha Huruma Missionary Sisters of Charity Hombolo Dodoma leo April 5, 2021.
Post a Comment