Featured

    Featured Posts

UWT DODOMA TUTAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA KUCHAPA KAZI, KUFUNGUA MIRADI YA THAMANI-MAJULE+video

 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Mkoa wa Dodoma, Neema Majule amesema kwa wamefurahi sana kuwa na Rais Mwanamke, Samia Suluhu Hassan na kwamba watamuunga mkono kwa kuchapa kazi na kufungua miradi yenye tahamani, ikiwemo mradi wa mgahawa wa kisasa na bucha ya kisasa yenye thamani ya sh. mil. 120, katika eneo lao la Kilimani jijini Dodoma.

Mdau nakuomba uendelee kuisoma taarifa na clip hii ya video Majule akielezea jinsi watakavyomuunga mkono mwanamke mwenzao Rais Samia...
Michoro ya miradi ya migahawa na bucha inayotarajiwa kujengwa eneo la UWT Mkoa Dodoma lililopo Kilimani.

     Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma, Neema Majule

HONGERA UWT MKOA DODOMA. 

Nachukua nafasi hii kwa niaba Kamati ya Utekelezaji Mkoa na kwa niaba yangu mimi mwenyewe   kuwapa tena pole kwa msiba mkubwa wa kuondokewa na aliyekuwa Rais wetu Hayati Mhe Dkt. John Pombe Joseph  Magufuli.

 Pia niwapongeze Sana wanawake tumepata chuma kingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwanamke mwenzetu Mwadilifu mchapa kazi, Jembe jingine Mama Samia Suluhu Hassan. 

Chini ya uongozi wake, Rais Samia wanawake tutarajie maendeleo makubwa sana. Pia niwapongeze viongozi wa Jumuiya yetu ya UWT Taifa Mhe. Mwenyekiti wetu Bibi Gaudentia Kabaka our role model na  Katibu Mkuu Mhe. Queen Mlozi dada yangu wanatuongoza vema  kwa Uongozi uliotukuka,  tuna mazingira mazuri ya kufanya kazi na kuleta maendeleo makubwa ya Wanawake. 

Ndoto zangu kama Mwenyekiti wenu  wa Mkoa ya kuukomboa Mkoa wetu kiuchumi zinaendelea kutimia. Asanteni kunipa kamati ya utekelezaji nzuri makini tunayoendana nayo kimaono na speed ya kupanga na kutekeleza mambo.

 Hayawi Hayawi yamekuwa. Tumepata Mwekezaji ambaye atatujengea majengo hayo mawili hapo Kilimani yatakayo kuwa mgahawa Resturant 2 za kisasa na bucha kubwa ya nyama (Morden Butcher).

 Hatua zote za uwekezaji zinekamilika Tarehe 1/4/2021 na ujenzi sasa utaanza mara atakaposaini mkataba mapema wiki ijayo. Vikao vyote kuanzia kamati ya utekelezaji ya UWT Mkoa, kamati ya siasa Mkoa. Idara ya uchumi na fedha Taifa, kitengo cha UWT Taifa uwekezaji vimetoa Baraka zake na vibali kazi Sasa  inaanza.  Mradi huu utagharimu million Mia moja ishirini na mbili  tu (122,000,000) za Kitanzania.
 
Hongereni wanawake UWT Dodoma tutalipwa kodi kila mwezi million 1 sawa na million kumi na mbili (12,000,000) kwa mwaka  na tutakabidhiwa jengo hili baada ya miaka 5 ni la kwetu. 

Sambamba na hilo mwekezaji anatupa million 15 sehemu ya kodi yetu mapema kuanzia sasa itakayotuwezesha kununua gari la UWT Mkoa aina ya Noah 4 wheel drive kama kamati yenu ya utekelezaji ilivyopanga. 

Gari hili zuri la UWT Mkoa litawezesha kamati ya utekelezaji kufanya ziara Mkoa mzima kuimarisha jumuiya kwa kuongeza idadi ya wanachama kutoka 95 000 hadi 150 000 ifikapo 2022  tuwafikie ndugu zetu wanawake tusikilize kero zenu na ili tubaini na kujenga  miradi ya kila wilaya. Pia ndio itakayokuwa Gari ya Katibu wetu wa UWT Mkoa.  

Pia  litasaidia kusafirisha wanafunzi wa shule yetu ya Kilimani. Pia niwape taarifa Shule yetu ya UWT  Mkoa inaendelea vizuri Sana Ina wanafunzi 22  hadi Sasa wataendelea kuongezeka kila siku. Kila mwanafunzi analipa 800 000 kwa mwaka  na tulipata Gari watalipa 1 200 000 kwa mwaka hivyo kuwawezesha nyie kupata  zaidi ya million 20 kwa mwaka tukiunganisha na Registration na uniforms. 

Pia frame zetu za maduka  block 1 Kilimani Tunapokea kodi za maduka 4 zinatuingizia million 12 kwa mwaka. Hivyo si haba wanawake wenzangu wa Dodoma tukiangalia tulikotoka na account zero au sufiri  Sasa tunaongelea mapato ya zaidi ya million 50 ya miradi yote kwa mwaka na Gari la UWT . Hivyo kwa ujumula Jumuiya yetu ya UWT Mkoa ipo vizuri. 

Tumefanya mengi na tunategemea  kufanya makubwa zaidi ya hayo. Endeleeni kutuombea kamati ya utekelezaji Mkoa na mimi Mwenyekiti wenu nawapenda Sana kila siku nawawazia nawatoaje hapo mlipo kwenda mahali pazuri zaidi kisiasa kiuchumi na kijamii.

Niwakaribishe kuja kuona maendeleo yenu makubwa baada ya miezi 2 jengo lenu kipya litakuwa tayari.

HONGERA TENA UWT MKOA WA DODOMA na nawatakia pasaka njema. 

Mwenyekiti wenu wa UWT  Mkoa 
Neema Majule.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
 MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
 0754264203
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana