Featured

    Featured Posts

UWT YATAKA WANAHARAKATI WA MASUALA YA WANAWAKE, WASOMI NA MAKUNDI MAALUM KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA

 

Rais Mama Samia

Na Antar Sangali, Zanzibar

Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa Kaskazini Unguja umesema sasa ni wakati muhimu kwa wanaharakati wa masuala  ya Wanawake,  Wanasiasa Wasomi na Makundi Maalum kumuunga mkono Rais  Samia  Suluhu Hassan kwa kuwa kitendo cha kupatikana kiongozi mwanamke  na kuwa rais  kihahitaji kushangiliwa kwa  shangwe la nguvu, ari na ujasiri.


Hayo yameelezwa na Mwenyekiti  wa UWT Mkoa Kaskazini Unguja Maryam Muharram  Shomari  akiwa Mahonda mkoa Kaskazini Unguka aliyesema ni fahari kwa Mama Samia kuwa Rais wa kwanza mwanamke Tanzania. 


Maryam amesema kumpata  Rais Samia  kuwa Mkuu wa nchi, kuzidishe mshikamano miongoni mwa wanawake viongozi wa kisiasa , madiwani, wawakilishi, wabunge na wanaharakati 


Amesema  huu ni muda muafaka wa kumuunga mkono Rais huyo kwa shangwe na vitendo vitakavyodhihirisha umoja na maendeleo  .


Mary amesema bila kujali  ni  vyama gani au makundi yepi ya kiharakati ,itikadi za kisiasa ziwekwe kando na wanawake wamlinde na kumtetea Rais  huyo


Ameeleza  bila kujali makundi ya wanasiasa wanawake au wasomi  waanze  kujadili vikwazo na chamgamoto  zinazowakabili  wanawakw kitaifa na kikanda.


Aidha Mwenyekiti  huyo amesema iwapo wanawake  watautumia vyema wakati kwa kushikamana,  kuzidisha juhudi ,bidii na maarifa, watawanusuru wanawake walioko mijini na vijijini 


Amewataka wanawake wenzake kila mmoja kwa wakati wake kuwa askari dhamana atakayelinda kiti cha urais wa mama  samia kwani dhamana  hiyo ni dhamana ya wanawake wote.


Maryam amengeza kusema kuwa itakuwa fedha ikiwa wanawake watasita kumtetea mwanzao ataposakamwa na watetea wa  mifumo kandamizi  badala yake wote  wasimame kidete


Hata hivyo  mwenyekiti huyo wa uwt mkoa kaskazini unguja amesema uamuzi Tanzania kumpata rais mwanamke ufunhue njia kwa afrika hatimaye kila nchi ifikirie na kuwaamini wanawake 

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana