Featured

    Featured Posts

MAFUNZO YA ULTRASOUND KWA WATAALAMU WA VIPIMO VYA MIONZI KATIKA TAASISI YA MIFUPA MOI YARINDIMA KWA SIKU MBILI

Raisi wa Chama cha wataalamu wa Radiorafia (Tanzania Association of Radioraphers) Tech Bakari Msongaamwanja akizungumza jambo katika Semina ya Wataalam wa Radioraphia (Ultrasound Workshop) iliyofanyika katika Ukumbi wa Taasisi MOI. Ambapo  mada mbali mbali zilijadiliwa ikiwemo, Uwasilishwaji wa mada zihusuzo,Upimaji wa kina mama wajawazito na watoto, Elimu kwa Vitendo pia ilitolewa ambapo kwa mwaka huu wanatarajia kufanya Semina kama hii Mwezi wa kumi na moja jiji Mwanza wakiwa wanaadhimisha Wiki ya Huduma za Radiologi Duniani. Zaidi ya nchi 20 kupitia njia ya mtandao (zoom meeting) zimeshiriki mafunzo hayo ambayo yatawezesha utoaji huduma za ultrasound bora na kubadilishana uzoefu. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

Makamu wa Rais Chama cha wataalamu wa Radiorafia, Mtaalamu tiba wa Saratani kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road. Jerome Jairos Msamba akiendesha mafunzo ya Ultrasound wakati wa semina hiyo.

Mkuu wa Idara ya Radiologia MOI. Dr. Mechris Mango akizungumza jambo katika Semina ya Wataalam wa ultrasound.
Baadhi washiriki wakisikiliza kwa umakini 

Dr Bingwa wa Mionzi Hospitali ya Agakhan Jijini Dar es Salaam akitoa mada katika semina hiyo

Wadhamini wa Semina hiyo kutoka Nchini China katika Kampuni ya Mindray inayo jihusisha na utengenezaji wa vifaa mbalimbali vya Uchunguzi na Tiba katika Sekta ya Afya 
Rais wa Wataalam wa Radiografia Tanzania (TARA) Tech. Bakari Msongamwanja (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Wataalam hao

Rais wa Wataalam wa Radiografia Tanzania (TARA) Tech. Bakari Msongamwanja akizungumza jambo wakati wa Semina hiyo mara ya kuulizwa swali na Mtaalam wa Mafunzo ya Ultrasound kutoka Kampuni ya Mindray iliyopo Nchini Kenya. Mary Goretty (kulia)

Mtaalam wa Radiographia Ms Begina Byela kutoka AghaKhan Hospitali ya jijini Dar es salam akitoa maada katika semina hiyo.

Mtaalam wa Radiographer Taasisi ya Mifupa MOI akizungumza jambo wakati wa Semina hiyo iliyo anza Mei  21-22, 2012  
Rais Mteule Chama cha Wataalam wa Afya ya Kinywa na MenoTanzania (TDA). Dr. Gemma Berege akitoa pongezi kwa Viongozi wa Chama hicho cha Wataalam wa Altrasound kwa kubuni mbinu mbalimbali na kuweza kuwa na mawazo mazuri ya kukiendesha Chama hicho kwa Utaalam wa hali ya juu na kuwapongeza washiriki wote waliofika katika Semina hiyo

Mtaalam wa Mafunzo ya Ultrasound kutoka Kampuni ya Mindray iliyopo Nchini Kenya akizungumza jambo katika mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku mbili

katibu wa Chama cha wataalamu wa Radiorafia,Omary Msehwa  akizungaumza na wanataaluma waliohudhuria mafunzo hayo.




author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana