Mbunge wa Jimbo la Chemba, Mohamed Moni amefanya mikutano ya hadhara katika Kata ya Lahoda vijiji vya Handa na Lahoda ikiwa ni mwendelezo wa ziara ambapo lengo ni kuwashukuru wananchi kwa kumchagua lakini pia kusikiliza kero zao.
Katika ziara hiyo aliyoifanya hivi karibuni, Mbunge Moni amewaomba wananchi kuendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi kwani bado ndiyo chama pekee chenye dhamira ya dhati ya kuwaletea maendeleo.
Mbunge Moni aliwaeleza alipata wasaa wa kuwaeleza wananchi mambo kadhaa ambayo kayafanya tangu achaguliwe kuwa mbunge.
Pamoja na mambo mengine, Mbunge huyo akiwa kijiji cha Handa aliwaeleza wananchi kuwa alishachangia sh.milioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati lakini pia amewezesha kupatikana milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa shule ya msingi na sh. milioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo.
Amewaomba wananchi kuzitumia fedha hizo vizuri ili ziweze kutumiza malengo yake.Hata hivyo akatoa msimamo "kuanzia sasa fedha zinazokuja kwa ajili ya maendeleo zitasimamiwa na wanakijiji husika kwani wao ndiyo walengwa na wadau wakuu" alisisitiza Moni kuhusu jambo hilo.
Post a Comment