Na Hamis Shimye
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM), kimesema kitaendelea kutetea makundi yote ya kijamii nchini ili yaweze kutatuliwa changamoto zao na kuzidisha imani waliyokuwa nayo kwa CCM.
Pia, imewataka viongozi wa kiserikali wa ngazi zote kujielekeza katika kutatua shida za wananchi ambao ndio wadau wakubwa wa uwepo wa Chama Cha Mapinduzi madarakani.
Hayo yamesemwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC)Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka wakati wa makabidhiano ya Ofisi baina yake na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC)Itikadi na Uenezi mstaafu Humphrey Polepole, leo katika Ofisi Ndogo ya Makao makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam.
Shaka amesema Chama kimejizatiti kuendelea kutatua shida za wananchi na kimeshatoa mwelekeo kupitia kwa Katibu Mkuu Daniel Chongolo, kwa kuwa CCM haitakuwa tayari kuona Watanzania wakihangaika,kutaabika na kukosa haki zao za msingi.
''Sekretarieti imeshatoa mwelekeo kwenye mkutano wa Katibu Mkuu Chongolo, kila kiongozi ngazi yeyote kuhakikisha anajielekeza katika kutatua shida za wananchi'', alisema.
Shaka alisema kila kiongozi katika taasisi za umma na za kiserikali kila moja kutimiza wajibu wake kwa kutumikia na kufuata miongozo ya kisera na malengo ya kimkakati yalioainishwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020.
"Wote ni mashahidi Rais Samia Suluhu Hassan amechukua jitihada za wazi za kujenga mahusiano mema, ikiwemo kuchochea biashara na uwekezaji'' alisema.
Shaka alisema ameondoa vizuizi vya kibiashara kwa manufaa ya wote na kuwahimiza wafanyabiashara na wananchi kulipa kodi na kodi isiwe bughudha na kuzuizi bali kila mmoja alipe kwa wakati na hiari.
Kwa mujibu wa Shaka, Rais Samia ana nia ya dhati na amekuwa na dhamira ya kujenga nchi huku akitaka iende kwa mwendo wa haraka ndio maana ameanza kufungua milango iliotaka kujifunga akifuata nyayo za watangulizi wake ambao wote walipikwa, kuandaliwa na kupewa dhamana ya uongozi na CCM.
Akizungumzia kukabidhiwa kwake ofisi na aliyekuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa(NEC), Humprey Polepole, Shaka alisema mabadiliko ni kawaida kutokea na wahusika kukabidhiana ofisi kwa mshikamano na umoja.
''Hii ndio ukomavu wa CCM, nakushukuru ndugu yangu Polepole, umefanya kazi kubwa na ninamatumaini utakuwa mwalimu wangu katika hii nafasi kwa kuwa nikifanya vizuri sifa ni zako na nikifanya vibaya nawe utahusika'' alisema.
Aliongeza ''Nakuomba ukiwa na jambo lolote la kuboresha ofisi hii, milango iko wazi mahala popote na sehemu yeyote nitakuja kukusikiliza na kuchukua mawazo''
Shaka alisema lengo ni kuhakikisha wanaijenga taasisi ya CCM kwa nguvu kubwa na kusimamia shabaha na malengo yake katika kuleta maendeleo kwa wananchi.
"Kwa dhamana nilionayo naahidi kuwa kiungo na daraja kwa watendaji wenzangu na makundi ya wanahabari, wanamichezo, wasanii na walemavu'' alisema
Alisema hilo linatokana na Rais Samia kusema upepo uwe mwingi au kidogo jahazi litatia nanga katika bandari ya mafanikio na wao kama Chama wanaunga mkono msimamo huo kwa kutekeleza kwa vitendo.
Naye, Polepole alisema anashukuru kukabidhi ofisi huku akimtaka Shaka kufanya kazi kwa bidii kwa kuwa anamuamini katika utendaji wa Chama kutokana na uzoefu aliokuwa nao toka alipokuwa kiongozi Umoja wa Vijana(UVCCM).
Aliyekuwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akimtwisha Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi mpya Shaka Hamdu Shaka, mzingo wa nyaraka mbalimbali za Ofisi ya Idara hiyo, wakati makabidhiano ya Ofisi, leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.Aliykuwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akizungumza wakati akimkabidhi Ofisi Katibu wa nec Itikadi na |Uenezi Shaka hamdu Shaka, leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka akitazama kwa makini moja ya hati za makabidhiano, wakati akikabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, leo
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka akitia saini nyaraka hati za makabidhiano moja baadab ya nyingine wakati akikabidhiwa ofisi na aliyekuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, leo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka akipokea hati za makabidhiano ya Ofisi wakati akikabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, baada ya wote kuzisaini hati hizo, leoKatibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka akizungumza wakati wa makabidhiano ya ofisi na aliyeliwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, Kushoto ni Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi Zakary Mwansasu.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka akifafanua jambo alipokuwa akizungumza wakati wa makabidhiano ya ofisi na aliyeliwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka akipokea miongoni mwa nyaraka za ofisi alizokabidhiwa, wakati akikabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, leo
Kisha polepole akamtisha Shaka mzingo wenye nyaraka zote. Kisha wakapeana mikono kwa kufanikisha makabidhiano hayo.
Baadhi ya Viongozi, Wafanyakazi na Waandishi walioshuhudia tukio hilo.
Katibu wa NEC Itikasi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka na aliyekuwa Katibu Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na Wafanyakazi wa Idara ya Uenezi, baada ya makabidhiano hayo.
b
Picha zote na Bashir Nkoromo
Post a Comment