Featured

    Featured Posts

SAMIA: VIFO VYA M-NEC MOROGORO NA MWENYEKITI UWT TABORA NI MSIBA MZITO

Makao Makuu ya CCM, Dodoma

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa ya vifo vya viongozi wake vilivyotokea jana Mei 18, 2021,  jijini Dar es Salaam na Morogoro.


Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka, imetaja vifo hivyo kuwa ni cha Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kutoka Mkoa wa Morogoro Hassan Masoud Mamba (Bantu) kilichotokea Hospitali ya Taifa Muhimbili na cha Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Tabora Mwajuma Muhina kilichokea katika Hospitali ya Wilaya Nzega.


Shaka amesema kwamba, Mwenyekiti  wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan amevitaja kwa pamoja vifo hivyo kuwa ni msiba mzito kwa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake kwa kuondokewa na viongozi hao wawili ambapo Chama kiliwategemea, kuwatumaini na kunufaika nao kwani walikuwa wanasiasa hodari, wazoefu na wachapakazi.


"Kazi ya Mwenyezimungu haina makosa, kufariki dunia kwao wakati huu ni jambo la kusikitisha kwani ni wakati ambao ushauri wao, upeo na maarifa waliyokuwa nayo katika kufanikisha kazi na mipango ya kisiasa, kioganaizesheni na kisera ilikuwa ni msaada mkubwa kwa Chama Cha Mapinduzi", Taarifa hiyo imemkariri Mwenyekiti wa CCM Rais Samia akisema na kuongeza kuwa;


"Chama Cha Mapinduzi kinatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wanachana wa CCM Mkoa wa Morogoro na Tabora kwa kuondokewa na Viongozi wetu wapendwa. Tunawaomba kuwa na uvumilivu, ustahamilivu na subira kwenye kipindi hiki kigumu cha maombolezo na mazishi.


Hakika Sisi ni wa MwenyeziMungu na Kwake ni Marejeo Yetu".

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana