Tarehe, 15.5.2021
Jimbo la Musoma Vijijini
EID AL FITR ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini husherehekewa KILA MWAKA kwa MISIKITI 3 kuandaa sikukuu hiyo. Jumla ya Misikiti Jimboni mwetu ni 37.
Kwa MWAKA HUU (2021) mzunguko wa MISIKITI 3 wa kila Mwaka umetua kwenye MISIKITI ya VIJIJI vya:
*Bukima
*Kiriba
*Kakisheri/Kigera
MADHEHEBU YA KIKIRISTO nayo husherehekea KRISMASI na PASAKA kwa mtindo huu huu wa mzunguko ndani ya VIJIJI 68 vya JIMBO la Musoma Vijijini.
UTARATIBU huu wa kuwaweka WANANCHI pamoja wakati wa SHEREHE za KIDINI na wakati wa KAZI za kujiletea MAENDELEO yao ni sehemu ya MPANGOKAZI wa MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo.
MASHINDANO YA KUHIFADHI QURAAN
*WAISLAMU wa Jimbo la Musoma Vijijini wameamua kutayarisha MASHINDANO hayo kwa kushirikiana na Mbunge wao wa Jimbo. Tarehe itapangwa.
SHEREHE za KIDINI, mbali ya kufanyika kwa TAFRIJA za pamoja, hutumika KUKUMBUSHANA UTEKELEZAJI ya MIRADI ya MAENDELEO ya KATA iliyoandaa SHEREHE kwa Mwaka huo.
(1) EID AL FITR KWENYE MSIKITI WA KIJIJI CHA BUKIMA
WANANCHI wamekumbushwa na kuhimizwa kukamilisha MIRADI ifuatayo:
(a) Wodi ya Mama&Mtoto ya Zahanati ya Bukima
(b) Ujenzi wa Vyumba vipya vya Madarasa kwenye Shule zote za Msingi na Sekondari yao.
(c) Kasi iongezwe kwenye ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Butata
(2) EID AL FITR KWENYE MSIKITI WA KIJIJI CHA KIRIBA
WANANCHI wamekumbushwa na kuhimizwa kukamilisha MIRADI ifuatayo:
(a) Ujenzi wa Vyumba vipya vya Madarasa na Ofisi za Walimu wa S/M Kiriba B. Shule hii inahama kutoka kwenye eneo la pamoja na S/M Kiriba A
(b) Kasi ya ukamilishaji wa Maabara, Vyumba vipya vya Madarasa na Jengo la Utawala la Kiriba Sekondari iongezeke.
(c) Kitongoji cha Kubuingi cha Kijiji cha Kiriba kianze ujenzi wa SHULE SHIKIZI. Watoto wao wanatembea umbali mrefu kwenda masomoni kwenye S/M Kiriba A&B
(3) EID AL FITR KWENYE MSIKITI WA VIJIJI VYA KAKISHERI NA KIGERA
*Vijiji 2 hivi vinatumia Msikiti mmoja ambao unaendelea kujengwa kwa msaada mkubwa wa MAMA DIBOGO wa Musoma Mjini.
*Ujenzi wa Jengo la Madrasa utaanza hivi karibuni.
*KASWIDA iliyoambatanishwa hapa imeimbwa na vijana wa Msikiti huu.
WANANCHI wamekumbushwa na kuhimizwa kukamilisha MIRADI ifuatayo:
(a) Kuongeza kasi ya ujenzi na ukamilishaji wa SEKONDARI MPYA, ya kisasa, (imefunguliwa mwaka huu – Kigera Secondary School) inayojengwa na Vijiji hivi viwili.
(b) Kasi iongezwe kwenye ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kakisheri
MIRADI INAYOFADHILIWA NA SERIKALI
Mbali ya kutoa mkono wa EID AL FITR, Mbunge wa Jimbo hilo ameongea na WANANCHI na kuwaelezea MIRADI mbalimbali (k.m. elimu, afya, maji, umeme, barabara za TARURA & TANROADS) itakayotekelezwa na SERIKALI kwa kutumia BAJETI ya Mwaka wa Fedha ujao, Mwaka 2021/2022.
Vilevile, MBUNGE huyo amesikiliza kero za Wananchi na kuzitatua.
SHEREHE NA MAENDELEO MUSOMA VIJIJINI:
TUENDELEE KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YETU KUCHANGIA MAENDELEO YETU – TUTAFANIKIWA!
Post a Comment