Na Jastin Cosmas, Kakonko
Wafugaji kutika nchini Burundiaia wamedaiwa kuingiza mifugo yao katika ardhi ya Tanzania, Wilayani Kibondo mkoani Kigoma.
Sintofahamu hiyo imeibuka wakati wa wananchi wakihoji katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Rusenga kata ya Gwanumpu wilayani Kakonko,ambapo wamelaani kitendo cha mashamba yao kuvamiwa na wafugaji kutoka nchi ya Burundi huku mazao yao yakihalibiwa na ng’ombe.
Wananchi hao wamesema kuwa, mwnyekiti wa kijiji cha Rusenga Evarist Ndumiwe alitoa aridhi kwa wafugaji wa Burundi bila kushirikisha wajumbe wa halmashauri ya kijiji hicho cha Rusenga.ambapo wajumbe wa kijiji hicho wamesema hawana imani na mwenyekiti huyo.
Nae mwenyekiti wa kijiji hicho Evarist Ndumiwe ametupilia mbali lawama hizo, akisema kuwa ameingia kwenye uongozi ng’ombe hao wakiwepo hivyo haja ruhusu ng’ombe hao kuingia Tanzania.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Gwanumpu Toyi Butono amesema kuwa ng;ombe hao waondolewe, sheria na taraibu zifatwe na aridhi iludishwe kwa wananchi.
Ntarabe Mvulugu, ni miongoni mwa wananchi ambao mashamba yao yamevamiwa ambapo amesema kuwa tayari mazao yake yamehalibiwa na ng’ombe, na hana sehemu nyingine yakulima kwani alikuwa anategemea sehemu hiyo kwa shuguli ya kilimo.
Mwenyekiti wa ulinzi na usalama ambae ni mkuu wa wilaya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amesema kuwa hajapata taarifa kuhusu kuwepo kwa ng’ombe hao hivyo suala hili atalifuatiria kwa kina
Wanachi wa kijiji cha Rusenga kata ya Gwanumpu wilayani Kakonko mkoani Kigoma, wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wakidai kurudishiwa aridhi yao iliyo chukuliwa na Raia wa Burundi ambao ni wafugaji
Post a Comment