Featured

    Featured Posts

ALIYEKUWA MWENYEKITI NA MFADHILI WA YANGA YUSUF MANJI AREJEA JIJINI DAR ES SALAAM

Yusuf Manji

Aliyekuwa Mwenyekiti na mfadhili wa  Klabu ya Yanga, Mfanyabiashara Bilionea na Diwani mstaafu wa Mbagala Kuu jijini Dar es Salaam, Yusuf Manji inaelezwa kuwa  amerejea Tanzania.


Chanzo cha uhakika kinasema  kuwa, Manji amereja nchini jana jioni na inaelezwa kuwa huenda ikawa ni neema kwa wadau wa soka nchini, kwani kuondoka kwake kulikuwa mwanzo wa Klabu ya Yanga kuyumba kiuchumi.


"Inawezekana ndiyo safari ya timu yetu nzuri iliyoanguka tangu mwaka 2015, Simba wakachukua nafasi, ikarejea tena. Inshallah, tunamuombea ndugu yetu heri aweze kuanza upya, tupo naye pamoja," kimedokeza chanzo hicho.


Imeelezwa kuwa baada ya Manji kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julias Nyerere amehojiwa na baadhi ya maafisa wa Uhamiaji juu ya uhalali wake wa kuingia nchini Tanzania, kishaa liachiwa baada ya maafisa hao kujiridhisha kuwa ni Mtanzania na alikuwa na haki ya kuingia nchini muda wowote.


Manji ni Mkurugenzi Mtendaji wa Quality Group Limited (QGL), kampuni binafsi  inayomilikiwa na familia ya Manji. 


Kulinganaa na wasifu wake, tajiri huyo ana ukwasi mkubwa wa fedha. Mafanikio yaliyotokana na stadi za kipekee katika usimamizi wa biashara baada ya kuchukua kampuni iliyokuwa ikijihusisha na magari ya baba yake jijini Dar es Salam mwaka 1995.


Baadaya kuichukua aliibadilisha kuwa Kampuni ya Kimataifa yenye mafanikio na inayofanya kazi katika Mataifa mbalimbali Duniani ikiwemo Tanzania yenyewe,Umoja wa Falme za Kiarabu, India na Kenya. 


Kampuni ambayo inaundwa na kampuni tanzu zaidi ya 10 ikijihusisha na uwekezaji katika magari,bidhaa za uhandisi, biashara za kimataifa, vifaa, mali zisizohamishika, usindikaji wa chakula, ushauri, usafirishaji, aluminium na sekta ya uvuvi.


Kampuni yake inakadiriwa kuajiri zaidi ya watu 3,500 ambapo unufaisha wategemezi 10,000 kila siku. Manji anatajwa kuwa mstari wa mbele kutoa udhamini kwa wanafunzi mbalimbali ikiwemo kusaidia misaada mingi kabla na baada ya matukio ya dharura katika jamii.

Chanzo: Matukio Daima

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana