Featured

    Featured Posts

BUNGE SPORTS CLUB YATWAA USHINDI WA JUMLA TAMASHA LA MICHEZO LA CRDB DODOMA+video

Wachezaji wa Timu za Bunge (Bunge Sports Club) wakiwa na furaha baada ya kuwa washindi wa jumla wa Tamasha la Michezo lililoandaliwa na Benki ya CRDB kwenye Uwanja wa  Jamhuri jijini Dodoma leo Juni 12 ambapo mgeni Raismi alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Timu za Bunge zilishinda michezo mbalimbali ikiwemo Netibali, Mpira wa Kikapu, kufukuza kuku, kuvuta kamba.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (kushoto) akimkabidhi Nahodha wa Timu za Bunge, Naibu Spika, Dkt Tulia Ackson kombe la ushindi wa jumla wa Tamasha hilo.
Naibu Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson akimkabidhi Nahodha wa Timu ya Bunge ya Mpira wa Kikapu, kikombe cha ushindi wa mchezo huo.
Mchezaji wa timu ya Bunge, Halima Mdee akifurahia zawadi ya kuku baada ya kuwa mshindi wa mchezo wa kufukuza kuku.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Utamaduni, Pauline Gekul (kushoto) akimkabidhi Nahodha wa Timu ya Soka ya Benki ya CRDB, Tully Mwambapa kombe la ushindi wa mchezo huo.

Wachezaji wa Timu za Bunge wakishangilia ushindi wa jumla
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapongeza wachezaji wa timu ya Bunge ya kuvuta kamba baada ya kuishinda  timu ya CRDB.
                                 Mchezo wa Pool

                             Mchezo wa Bao
Ilikuwa ni mbilingembilinge wakati timu ya Bunge ilipokuwa ikichuana na timu ya Benki ya CRDB  wakati wa Tamasha hilo. Timu ya CRDB ilishinda kwa mikwaju ya penalti.
Wachezaji wa timu ya Benki ya CRDB (RANGI YA KIJANI) wakichuana vikali katika mchezo wa Netiboli. Timu ya Bunge ilishinda.
Mbunge wa Malinyi, Antipas Mgungusi akiwaongoza wabunge wenzie kuvuta kamba dhidi ya timu ya Benki ya CRDB. Timu ya Bunge ilishinda.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kagera, Neema Rugangira akiongoza wabunge wenzie katika shindano la kuvuta kamba dhidi ya Timu ya wanawake ya Benki ya CRDB. Bunge ilishinda.
Mashabiki wa timu ya Bunge wakishangilia baada ya kushinda mchezo wa kuvuta kamba dhidi ya CRDB.
                             Mchezo wa Drafti
                                    Mchezo wa Bao
                                 Mchezo wa Karata
Mchezaji wa Bunge Sports, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete akipiga penalti dhidi ya timu ya Benki ya CRDB.

 Wakishindana katika mchezo wa kukimbia na gunia.

PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA 

 

Mdau, nakuomba uendelee kuona kupitia clip hii ya  video yaliyojiri kwenye tamasha hilo.....

 

Mhariri Blog ya Taifa ya CCM

0754264203

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana