Featured

    Featured Posts

CCM YAOMBOLEZA KIFO CHA MAMA VICKY NSILO SWAI, RAIS SAMIA ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI

CCM Blog, Dar es Salaam

Chama Cha Mapinduzi(CCM) kimesema kimepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa kifo cha mwanasiasa mashuhuri aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Kilimanjaro Vicky Nsilo Swai kilichotokea jana Mei 31,2021.

Taarifa ya CCM iliyotolewa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka imesema kuwa Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Samia Suluhu Hassan amemtaja marehemu Vicky Nsilo Swai kama mwanasiasa mahiri, mpambanaji, mwenye msimamo thabiti wakati wa uhai wake na alikuwa mstari wa mbele kupigania usawa wa kijinsia, utu na hadhi ya  mwanamke.

“Marehemu Mama Vicky ametumia sehemu kubwa ya uhai wake kuwaunganisha Wanawake wa Tanzania na kuwahimiza katika kushiriki shughuli za maendeleo kisiasa, kijamii na kiuchumi, “amesema Rais Samia Suluhu Hassan kupitia taarifa hiyo ya CCM.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Vicky Nsilo Swai amewahi pia kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Kilimanjaro.

 Aidha, akiwa Mke wa Muasisi wa Chama, Marehemu Asanterabi Zephaniah Nsilo Swai, Mama Vicky ameshiriki katika harakati za ukombozi wa Tanganyika pamoja na kusaidia ukombozi wa mataifa mengine kusini mwa Bara la Afrika.

“Miongoni mwa sifa kubwa alizowahi kuwa nazo Marehemu Vicky Swai, ni uaminifu, ambapo amewahi kuhifadhi viatu vya Mpigania Uhuru na Rais wa Kwanza wa Afrika Kusini Hayati Mzee Nelson Mandela kwa miaka 33 kuanzia mwaka 1962. vilipoachwa na mpiganaji huyo wa ANC kwa familia ya Mzee Asanterabi Nsilo Swai na kuvikabidhi kwake mwaka 1995 akiwa Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kusini.”

Hivyo Mwenyekiti wa CCM, Rais  Samia ametoa salamu za rambirambi na pole kwa familia ya marehemu Vicky Nsilo Swai na kuwaomba kuwa wavumilivu, wastahamilivu na wenye subira katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.

Mama Vicky Nsilo Swai (Kushoto), akiwa na Mama Maria Nyerere enzi za uhai wake.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana