Featured

    Featured Posts

NYONGO AITAKA SERIKALI KUWASAIDIA WABUNIFU KUPATA HAKI MILIKI+video

 

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Prof. John Kandoro (kulia) na Katibu Mtendaji wa NACTE, Dkt. Adolph Rutayuga (wa pili kushoto) wakiiongoza kamati ta kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ilipotembelea maonesho yaliyoandaliwa na NACTE kwenye viwanja vya Jamhuri  jijini Dodoma. Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Stanslaus Nyongo.

Mhadhiri wa chuo cha Mipango Dodoma Dkt Bonamax (kulia) Mbasa akitoa maelezo kwa kamati ya kudumu ya Bunge, Huduma na Maendeleo ya Jamii ilipotembelea banda la chuo hicho kenye maonesho ya vyuo vilivyo chini ya NACTE yanayoendelea kenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma

Mshirika wa Programu ya Uzamili, Bw. Simon Mukajanga (kulia) akizungumza na kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya jamii ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Stanslaus Nyongo (kushoto) ilipotembelea maonesho ya elimu ya ufunzi na mafunzo iliyoandaliwa na NACTE kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

 

 Na Mwandishi Wetu, Dodoma.

Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Huduma na maendeleo ya jamii Mhe. Stanslaus Nyongo ameshauri serikali iwasaidie wabunifu nchini kupata haki miliki za kazi zao ili kulinda haki zao.

 

Mhe. Nyongo ameyasema hayo jijini Dodoma baada ya kutembelea maonesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi na kujionea ubunifu wa kipekee uliofanywa na wanafunzi wa vyuo vilivyo chini ya NACTE, ambao wamebuni vitu mbalimbali vifaa vinavyoonesha kiasi cha geni ya kupikia iliyobaki kwenye mtungi na kutoa taarifa kielektroniki.

 

Amesema bila kulina ubunifu unaofanywa na vijana pamoja na abunifu wengine, utawakatisha tamaa wananchi kushiriki kwenye ubunifu na kwamba inawezekana pia mtu wa nchi nyingine aakaiba na kujitangaza kuwa yeye ndiye aliyebuni na kuchukuahaki ambazo siyo zake.

 

Aidha mwenyekiti wa huduma na maendeleo ya jamii amesema, kamati yake itahakikisha inakutana na mamlaka zinazotoa haki miliki ili kuhakikisha vijana waliobuni bidhaa hizo watambuliwe na kupewa hati miliki.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Tifa la Elimu ya Mafunzona Ufundi Prof. John Kandoro amesema Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Anthony Mtaka amesema anataka kukutana na wabunifu wote wanaoonyesha bidhaa zao kwenye manenesho yaliyoandaliwa na NACTE pamoja na taasisi za fedha ili kuangalia namna ya kuwasaidia.

Mdau nakuomba uendelee kusikiliza clip hii ya video Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Nyongo akizungumza baada ya kutembelea maonesho hayo...

 

Imeandaliwa na Richard Mwaikenda

 Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 

 0754264203

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana