Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Bungeni, Shally Raymond akiongoza semina hiyo.
Maofisa wa Bunge wakifuatilia kwa makini mada iliyokuwa inatolewa na Dkt Tulia kuhusu mavazi yanayotakiwa kuvaliwa bungeni.
Dkt Tulia akielekezaja jambo na Shally Raymond
Wabunge wakiwa makini kusikiliza mada zilizokuwa zinatolewa wakati wa semina hiyo.
Na Richard Mwaikenda, Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amefungua semina ya Chama cha Wabunge Wanawake juu ya uongozi na ushiriki wao bungeni iliyoandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwenye Ukumbi wa Msekwa Bungeni Dodoma leo Juni 6,2021.
Baada ya kufungua semina hiyo iliyoongwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kilimanjaro, Shally Raymond, Dkt Tulia alitoa mada ya jinsi ya kufuata Kanuni za Bunge na jinsi ya kuwafanya wawe maarufu kwa kuchagua ajenda za kutambulika anapochangia bungeni kama vile, ukatili uliopo katika jamii , mazingira, unyanyasaji wanawake na watoto, kuvaa nguo zisizofaa.
Pia alisisitiza wabunge hao wanawake kuuheshimu muda katika shughuli na matukio mbalimbali anayoyafanya ikiwemo bungeni ii kujiongezea thamani."Tujifunze kutunza muda".
Mada zingine ni kuwa na Tabia nzuri na Nidhamu, kuangalia mazingira na suala la mavazi yanayofaa kuvaliwa bungeni mahali ambapo ni pa uongozi na muhimu, hivyo amewataka wabunge kabla hajaondoka nyumbani wakijiandaa kwenda bungeni ajiulize endapo akiwa bungeni na ghafla akateuliwa na Rais na kutakiwa muda huo huo aende kuapishwa je kwa nguo aliyovaa anastahili kwenda au arejee nyumbani kubadilisha?
Kama anaona haifai basi kabla ya kuondoka nyumbani anatakiwa avae nguo inayofaa.
Katika semina hiyo mtoa mada mwingine alikuwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira ambaye alitoa mada kuhusu Uongozi wa Mwanamke, nini ajenda ya vyama vya siasa kuhusu wanawake? wanawake wanaona fursa na changamoto zipi?
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza clip hii ya video ujue yaliyojiri kwenye semina hiyo.
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
Post a Comment