Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), Anthony Temu akielezea umuhimu wa wananchi 100 wa Kijiji cha Mkundi, Kata ya Dumila, wilayani Kilosa, Morogoro kushiriki kazi ya kupima mashamba yao ya kilimo cha miwa ili wapate hati miliki za kimila.
Temu aliwaeleza kuwa wakipata hatimiliki za kimila wataweza kuzitumia kuweka kama dhamana kukopa fedha benki na taasisi zingine za fedha zitakaowaidia kupanua kilimo cha miwa na kuboresha miradi yao mingine.
Aliyazungumza hayo wakati wa kikao cha halmashauri ya Kijiji cha Mkundi na wakati wa Mkutano wa hadhara wa wananchi wa Kijiji hicho, ambapo waliukubali mpango huo kwa kauli moja na kuishukuru Mkurabita kwa kuwakumbuka na kuuomba uongozi wa Mkurabita kupima pia mashamba mengine zaidi.
Wajumbe wa Halmahauri Kuu ya Kijiji wakiwa meza kuu pamoja na uongozi wa Mkurabita na maafisa wa Halmashauri ya wilaya ya Kilosa wakati wa mkutano wa hadhara wa Kijiji.
Sehemu ya wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.
Viongozi wa Kijiji wakiangali ramani ya Kijiji ch Mkundi katika hati waliyokabidhiwa kutoka wilayani.
Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati wa mkutano wa hadhara.
Mwenyekiti wa Kijiji ch Mkundi, Boniventure Flawan akiwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika kazi ya upimaji wa ardhi.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mkundi, Martine Mshanga akifafanua jambo wakati wa mkutano wa hadhara.
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM.
0754264203
Post a Comment