Featured

    Featured Posts

LUGODALUTALI MUFINDI WAISHUKURU MKURABITA KUPATIWA MIZINGA 30 UFUGAJI NYUKI+video


Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), Anthony Temu (wa pili kulia) na Diwani wa Kata ya Igombavanu, Veronica Kilongumtwa (kulia) wakikabidhi moja kati ya mizinga 30 kwa Kikundi cha Watumia Maji wa Kijiji cha Lugodalutali, wikayani Mufindi kwa ajili ya ufugaji wa nyuki kijijini hapo.

Makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiuchumi wanufaika 395 wa Mkurabita wenye hati za miliki za kimila.

Wanachama wa kikundi hicho walionesha furaha yao kupata msaada huo na kuishukuru Mkurabita ambapo waliahidi kuutunza mradi huo ili ulete mavuno bora ya asali na mazao mengine kama vile nta, chavua na sumu ya nyuki ambayo yana bei nzuri katika soko.

Sehemu ya mizinga ikiwa imehifadhiwa katika Ofisi ya Kijiji cha Lugodalutali.
Kwaya ya Mashahidi wa Uganda ambayo kwa asilimia kubwa imeundwa na wanachama wa Kikundi cha Watumia Maji, kikitumbuiza wakati wa mafunzo hayo.

Afisa Ufugaji Nyuki wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Hassan Kapilima akitoa mafunzo kuhusu ufugaji bora wa nyuki wakati mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wa kiuchumi wananchi wa Kijiji cha Lugodalutali.

 

Mdau nakuomba uendelee kuona/kusikiliza kupitia clip hii ya video ujue yaliyojiri wakati wa makabidhiano hayo.....

Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203


 

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana