Featured

    Featured Posts

MAKAMU WA RAIS DK. MPANGO AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA BURUNDI NCHINI HUMO, LEO

Rais wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango Ofisini kwake Ikulu Gitega Burundi kwa ajili ya Mazungumzo. Makamu wa Rais  Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amemuwakilisha Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye kumbukizi ya kutimiza Mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa Rais wa Burundi Hayati Pierre Nkurunziza iliyofanyika jana katika Mji Mkuu wa Serikali Gitega Nchini Burundi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akizungumza na Mhe. Evariste Ndayishimiye Rais wa Burundi alipotembelea Ofisini kwake Ikulu Gitega Nchini Burundi, wakati Makamu wa Rais Dkt. Mpango alipomuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye kumbukizi ya kutimiza Mwaka mmoja tokea kifo cha aliyekuwa Rais wa Burundi Hayati Pierre Nkurunziza iliyofanyika jana katika Mji Mkuu wa Serikali Gitega Nchini Burundi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango, akiagana na Baadhi ya Watumishi wa Taasisi za Serikali ya Burundi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Melkior Ndadaye Bujumbura Burundi, alipokuwa akirejea Nchini Baada ya kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye kumbukizi ya kutimiza Mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa Rais wa Burundi Hayati Pierre Nkurunziza iliyofanyika jana katika Mji Mkuu wa Serikali Gitega Nchini Burundi.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana