Mbunge wa Kilombero, Abubakar Asenga akichangia mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii katika mkutano wa 12 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano jijini Dodoma, ambapo aliiomba serikali kuruhusu kipande cha ardhi cha hifadhi ya Taifa chenye urefu wa mita 50 eneo la Mang'ula Corner ijengwe barabara, ombi ambalo Waziri wa wizara hiyo, Dkt. Damas Ndumbaro aliruhusu kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbunge Assenga akimshukuru Waziri wa Maliasili na Utalii , Damas Ndumbaro kuruhusu kipande cha ardhi cha Mang'ula Corner kujengwa barabara.
Pamoja na mambo mengine, Assenga ameishauri serikali kupitia wizara hiyo kuweka picha za Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere na Rais wa sasa, Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kumbukumbu na utambulisho wa Taifa letu.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Mbunge Assenga akizungumzia mambo hayo....
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
Post a Comment