Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani Benki ya NMB – Benedicto Baragomwa, akikabidhi funguo ya gari la mizigo aina ya Tata Ace ‘kirikuu’ kwa mshindi wa droo ya mwezi wa pili ya ‘NMB Bonge la Mpango’, Paulo Swai (kulia), wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika tawi la NMB Tandika jijini Dar es Salaam . Wakishuhudia ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam-Donatus Richard (katikati) na Meneja wa tawi la NMB Tandika- Ahmed Nassor wa pili kushoto.
Mshindi wa mwezi wa pili wa kampeni ya NMB Bonge la Mpango, Paulo Swai kutoka Tandika- Dar es Salaam akifungua gari la mizigo aina ya Tata Ace ‘kirikuu’ baada ya kukabidhiwa funguo na Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani Benki ya NMB – Benedicto Baragomwa. Wakishuhudia ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam-Donatus Richard (pili kushoto) na Meneja wa tawi la NMB Tandika- Ahmed Nassor.
**********************************
Mkazi wa Temeke jijijni Dar es Salaam, Paulo Swai, ameshinda gari aina ya TATA ACE maarufu kama ‘Kirikuu’ lenye thamani ya Sh. Milioni 25 kupitia kampeni ya ‘Bonge la Mpango’ inayoendeshwa na Benki ya NMB.
Bwana Paulo amekuwa mtu wa pili kujishindia zawadi ya gari aina ya TATA AC tangu kuanza kwa kampeni hiyo Februari mwaka huu. Bonge la Mpango ni kampeni inayolenga kuhamasisha utamaduni wa kuweka fedha benki kwa wananchi wakiwemo wateja wa benki ya NMB kwa ajili ya akiba ya baadae.
Akizungumza kabla ya kukabidhi Kirikuu hiyo, Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa NMB – Benedicto Baragomwa alibainisha kuwa, NMB Bonge la Mpango imewanufaisha wateja wengi miongoni mwao, wamejishindia pesa taslimu, pikipiki za mizigo aina ya Lifan Cargo, Kirikuu na zawadi katika fainali itakuwa gari la kifahari aina ya Toyota Fortuner lenye thamani ya Sh. Milioni 169.
Kwa upande wake, Bw. Paulo aliishukuru benki ya NMB kwa zawadi hiyo na kuahidi kuitumia Kirikuu hiyo kama nyenzo ya kujipatia kipato.
Kampeni hii ya Bonge la Mpango ikiwa inaelekelea ukingoni ‘Grand Finale’, imeendelea kusisisitiza wateja wao kuendelea kuweka akiba na kufungua akaunti mpya, ili sio tu kushindania zawadi, bali kujiwekea akiba kwa maendeleo yao lakini pia kunufaika na huduma na bidhaa bora zinazotolewa na benki hiyo kubwa hapa nchini.
Post a Comment