Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wanawake wa Mkoa wa Dodoma kwa niaba ya wanawake wote nchini kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma..
Rais Samia ambaye ni mwanamke wa kwanza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, amewaahidi wanawake kuwa Mungu akimjalia atajitahidi ifikapo mwaka 2025 uwiano wa uongozi nchini uwe sawa kwa kuwa na asilimia 50 kwa 50 kwa wanawake na wanaume.
Pia, ameahidi kuzitekeleza kero nyingi zinazowakabili wanawake ambazo ni tatizo la upatikanaji wa maji, masuala ya afya vikiwemo vifaa tiba, elimu, upungufu wa walimu, mikopo kwa wanawake, mila potofu zinazowakandamiza wanawake pamoja na uwiano usiolingana katika uongozi.
Rais Samia amesema atajikita kusimamia majukwaa ya wanawake ambayo alidai yanasaidia sana kwa wanawake kukaa , kujadili mchangamoto zinazowakabili na kuzitafulia ufumbuzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akishukuru baada ya kukabidhiwa zawadi na wanawake wakati wa mkutano ambapo alizungumza na wanawake wa Mkoa wa Dodoma kwa niaba ya wanawake wote nchini.
Sehemu ya umati wa wanawake.
Msanii Zuhura Kopa maarufu kwa jina la Zuchu akitumbuiza kwa wimbo wake wa Suger Sukari.
Wanawake wakicheza wimbo wa Suger Sukari wa Msanii Zuchu
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Songwe, Neema Mwandabila (katikati) akijumuika na wanawake wenzie kucheza muziki wakati wa mkutano huo.
Ni furaha iliyoje.
Wakiimba wimbo wa Taifa
Rais Samia akiitunza fedha kwaya iliyokuwa ikitumbuiza wakati wa mkutano huo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, Dkt. Doroth Gwajima akizungumza maneno ya utangulizi akijiandaa kumkaribisha Rais Samia kuzungumza na wanawake.
Ilikuwa ni Bashasha tele.
Mbunge wa Nsimbo, Anna Lupembe (kushoto) na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Mahawanga wakisikiliza kwa makini wakati Rais Samia akihutubia.
Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji la CCM Mkoa wa Singida, Grace Mkoma akifurahia jambo wakati Rais Samia akihutubia
Rais Samia akimtunza Msanii wa muziki wa taarabu, Sabaha Salumu.
Rais Samia akiwaaga wanawake baada ya mkutano kumalizika.
Msanii wa muziki wa Taarab,Sabaha Salumu (kulia) akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma,Dkt. Fatuma Mganga (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda baada ya mkutano kumalizika. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Post a Comment