Featured

    Featured Posts

WAZIRI NDALICHAKO AAGIZA WAAJIRI KUWAPA NAFASI WANAFUNZI KUFANYA MAFUNZO KWA VITENDO

 

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati akifunga  maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yaliyokuwa na lengo kuonyesha bidhaa za elimu ya ufundi, yaliyomaliza leo Juni 2,2021 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,Mwalimu Josephat Maganga,akizungumza wakati wa kufunga maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yaliyomaliza leo Juni 2,2021 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt .Adolf Rutayuga, akizungumza wakati waa kuhitikishwa kwa  maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) kwa lengo kuonyesha bidhaa za elimu ya ufundi,yaliyomalizika leo Juni 2,2021 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi NACTE John Kondoro, akielezea jambo kwa washiriki wakati wa kuhitimishwa kwa maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) kwa lengo kuonyesha bidhaa za elimu ya ufundi,yaliyomalizika leo Juni 2,2021 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Francis Nanai ,akizungumza wakati wa kuhitimishwa kwa maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) kwa lengo kuonyesha bidhaa za elimu ya ufundi,yaliyomalizika leo Juni 2,2021 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Baadhi ya wanannchi waliohudhuria Maonyesho hayo wakifatilia hotuba ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) wakati akifunga  maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yaliyokuwa na lengo kuonyesha bidhaa za elimu ya ufundi, yaliyomaliza leo Juni 2,2021 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi tuzo ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yaliyokuwa na lengo kuonyesha bidhaa za elimu ya ufundi, yaliyomaliza leo Juni 2,2021 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako,akipokea zawadi yake aliyopewa na wanafunzi wa UDOM mara baada ya kufunga maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yaliyokuwa na lengo kuonyesha bidhaa za elimu ya ufundi, yaliyomaliza leo Juni 2,2021 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.

…………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ametoa wito kwa waajiri nchini kutoa nafasi kwa wanafunzi wa vyuo vya ufundi kufanya mafunzo kwa vitendo kwenye maeneo yao ya kazi ili kuwaandaa kabla hawajapata soko la ajira.
 
Wito huo ameutoa leo Juni 2,2021  jijini Dodoma wakati akifunga Maonesho ya Pili ya Elimu ya Mafunzo na Ufundi Prof.Ndalichako amesema kuwepo kwa ushirikiano kutaondoa changamoto kubwa wanayokutana nayo wamiliki wa vyuo ya kupata sehemu ya kuwezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo.
 
“Baadhi ya waajiri wamekuwa na matazo hasi na kukukataa kuwapokea wanafunzi kwa madai kuwa wanawapotezea muda kwa sababu wanaona kama bado hawajaiva hivyo naomba muone umuhimu wa kuwapatia nafasi ya  mafunzo kwa vitendo na kuwafanyia tathimini kabla hawajamaliza .” Amesema Prof Ndalichako.
 
Amesema kupitia fursa ambazo zinatolewa na waajiri kama kutakuwa na mapungufu kwa wanafunzi wanaporudi vyuoni kabla ya kumaliza mafunzo yao vyuo vitachukua hatua za kurekebisha na italeta manufaa zaidi kwa waajiri.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi NACTE John Kondoro,amesema kuwa kufanyika kwa maonesho haya kunasaidia kuchochea ustawi wa sekta ya elimu na mafunzo ya ufundi nchini na yamewezesha wananchi kuona mchango mkubwa unaotolewa na vyuo vya ufundi katika kuandaa raslimali watu itakayotumika katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.
 
Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mwalimu Josephat Maganga ameziomba taasisi zinazotoa mikopo kuona namna ya kutanua wigo wa kuwasaidia vijana wanaobuni vitu mbalimbali kuweza kupata mitaji.
 
Awali Katibu Mtendaji wa Baraza la Vyuo vya Ufundi Nchini (NACTE), Dkt.Adolf Rutayuga amesema kuwa  maonyesho hayo yamekuwa na mwitikio mkubwa kwani mwaka huu Taasisi 151 zimeshiriki tofauti na mwaka 2019 ambapo Taasisi 139 zilishiriki.
 
Dkt.Rutayuga amesema kuwa takwimu inaonyesha kuwa jumla ya wananachi waliotembelea mabanda imeonyesha kuongezeka kutoka watu 14,500 mwaka 2019 hadi 14,730 mwaka huu.
 
Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Francis Nanai  amesema sekta Binafsi imekuwa ikitoa nafasi za mafunzo kwa vitendo na itaendelea kupokea vijana wengi zaidi kujifunza kwa vitendo.
 
Aidha Nanai ameiomba serikali kuanzisha chombo cha juu cha kuratibu suala zima la kukuza na kuendeleza ujuzi nchini  na pamoja na kulinda maslahi ya Taifa na ajira za vijana wa kitanzania kuangalia upya masharti ya vibali vya ajira za kazi.
 
Naye Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Amani Kakana,ambaye ni mshindi wa jumla wa  maonyesho,  amesema hawatabweteka katika ushindi huo na wataendelea kuongeza juhudi kutatua changamoto katika jamii.
 
 
Maonesho ya Pili ya Elimu ya  Mafunzo na Ufundi yamefanika Jijini Dodoma kuanzia Mei 27 hadi Juni 2, 2021 na yameshirikisha Taasisi 151. Kauli mbiu ya Maonesho hayo ni “Kuimarisha Ushirikiano na Wadau katika Kukuza ujuzi kwa Maendeleo ya Viwanda”
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana