Featured

    Featured Posts

MBUNGE KAMONGA AAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO SHULE YA KETEWAKA LUDEWA

 

Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga
akiwa kwenye moja ya darasa la shule ya sekondari ya ketewaka iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe alipofanya ziara ya kutambua changamoto za shule hiyo na kutafuta njia ya kuzitatua

Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga
akiwa kwenye shule ya sekondari ya ketewaka
iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe
.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MBUNGE wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga
amejipanga kuhakikisha kuwa anatatua changamoto za shule ya sekondari ya ketewaka iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe ili kuhakikisha
wanafunzi wanafa vizuri kwenye masomo yao.

Akiwa kwenye ziara ya kutembelea shule
hiyo, alisema kuwa ameziona changamoto za bweni, ukarabati wa madarasa hivyo atalifikisha katika baraza la madiwani pamoja na kutafuta wadau watakaoweza
kusaidia ujenzi wa mabweni na ukarabati wa vyumba vya madarasa

Alisema kuwa vyumba vya madarasa vya shule
hivyo havina madirisha hali inayohatarisha afya za wanafunzi kutokana na baridi kali linalotokana na jiografia ya jimbo lake na mkoa wa Njombe kwa ujumla kuwa
na baridi kali.

Mbali na changamoto hiyo ya uhaba wa
mabweni lakini pia shule hiyo inakabiliwa na changamoto zingine kama ubovu wa vyoo, ukosefu wa Maji ya uhakika na Vitabu vya kiada na ziada jambo linalorudisha nyuma kiwa ngo cha elimu shuleni hapo.

Uamzi wa kutatua changamoto za shule
hiyo umetokana na wanafunzi kukabiliwa na tatizo la Magonjwa ya kuambukizana na mrundikano mkubwa wa wanafunzi  kwa kukaa chumba kimoja zaidi ya wanafunzi
125. 

Akizungumza wakati wa ziara ya mbunge
wa jimbo la Ludewa,mwalimu mkuu wa shule ya Kitewaka wilayani Ludewa Mkoa wa Njombe Mosela Mgaya alisema uwezo wa bweni ni kukaa wanafunzi 45 lakini kwa
sasa wanafunzi wanaotumia bweni hilo ni 125 hali inayochangia kwa kiasi kikubwa kuambukizana magonjwa yakiwemo Magonjwa ya Ngozi

 Alisema changamoto hiyo imekuwa ni  kilio kikubwa  kwa  wanafunzi wa shule hiyo kwakuwa ,shule inabweni moja lenye uwezo wa kubeba wanafunzi 48 lakini kutokana na wingi wa wanafunzi wamelazimika kuwaweka wanafunzi zaidi ya mia moja hali inayohatarisha afya zao.

 Alisema kutokana na kuwaepusha wanafunzi wasichana kukutana na changamoto ya kukatishwa masomo kutokana na
ujauzito wanaoweza kupata kutokana na kutembea umbali mrefu walilazimika kuwaweka wasichana bwenini huku wavulana wakisali nyumbani.

Aidha Mgaya alisema kuwa Mkusanyiko huo
wa wanafunzi katika bweni Moja unachangia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kuambukizana magonjwakwa ya Ngozi ambapo kwa sasa robo ya wanafunzi wanaolala katika bweni hilo wameanza kuugua ugonjwawa Ngozi.

 Fidea steven na Steria Haule ni wanafunzi wa shule ya sekondari Kitewakwa walikili kukabiliwa na changamoto
hiyo na kuiomba serikali na wadau wa elimu kuwasaidia kujenga bweni linguine litakalo waondolea adha ya mlundikano sambamba na kuwaondolea magonjwa ya
kuambukizana.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana