Featured

    Featured Posts

AY AKUBALI KUWA BALOZI WA KIJIJI CHA WASANII MKURANGA


Wasanii maarufu nchini Ahmed Olotu (Chilo) kulia na Ambwene Yessayah (AY) wakisikiliza mikakati yamaendeleo ya kijiji cha wasanii Mwanzega, Mkuranga.

Wachezaji na wasanii wa kijiji cha Mwanzega wakifurahia jezi za Simba na Yanga zilizotolewa na Kampuni ya Issere Sports.



Mkuu wa wilaya ya Mkuranga, Philberto Sanga akiwathibitishia wasanii kukuza michezo kwa kuwakabidhi mipira kwa ajili ya wachezaji chipukizi Mwanzega.


 Na Peter Mwenda

MWANAMUZIKI nguli wa kizazi kipya Ambwene Yassayah (AY) ameahidi kuwarudisha wanamuziki wenzake kama balozi mpya wa wasanii wa fani mbalimbali kwenye kijiji cha wasanii Mwanzega, Mkuranga.

Mwanamuziki hiyo  aliyewawakilisha Joseph Haule (Profesa J),Fareed Kubanda (FED Q),Hamisi Mwinjuma (Mwana FA) alisema kijiji cha wasanii kitawakomboa wasanii wakiwekeza Kijijini.

"Mimi na wasanii wenzangu tulikuwa waanzilishi wa kijiji hiki (2010) miaka kumi iliyopita tulijisahau lakini sasa tunarudi kwa nguvu zote kuhakikisha yale tuliyoyaanzisha tunayasimamia"alisema AY.

Mkuu wa wilaya ya Mkuranga akizungumza baada ya mwanamuzi AY kutambulishwa ofisini kwake Mkuu wa WIlaya Sanga  aliahidi kutimiza ahadi kwa kijiji cha wasanii Mwanzega kwa miundombinu ya barabara,Umeme na nani said na Salama.

Sanga aliahidi ukamilishaji huo mbele ya Mkurugenzi wilaya hiyo Injinia Mshamu Munde alisema wilaya itahakikisha kutoa ushirikiano wa kisanii na jamii.

Mkuu wa wilaya akipokea jezi za Simba na Yanga kwa vijana wa kijiji cha wasanii alisema michezo ni Afya hivyo anampongeza mwanachama Issere Sports kutoa vifaa hivyo vya michezo.

Mwenyekiti wa SHIWATA,Deo Kway alisema mtandao huo imeanza kutoa maeneo ya wazi yaliyotengwa kwa ajili ya wawekezaji wa sanaa mbalimbali.

Mwenyekiti Deo alisema SHIWATA mbali ya wasanii  wanachama kukamilisha ujenzi nyumba zaidi ya 250 pia ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa kuongeza watu 2,000 kwa pamoja baada kukabidhiwa ramani ya ukumbi huo.

Msanii maarufu Ahmed Olotu ( Chilo) aliwashauri wasanii wanachama wa SHIWATA qaliofanikiwa kimaisha warudi kuwekeza Kijijini kujenga hosteli za  wasanii wapate mafunzo kuandaa chipukizi wapya wa baadaye.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana