Kisutu, Dar es Salaam, leo
Mfanyabiashara maarufu hapa nchini James Rugemalira aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, akituhumiwa kujipatia fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow leo ameachiwa huru na Mahakama hiyo kufuatia Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kufuta mashtaka dhidi yake kwa sababu hana nia ya kuendela na mashtaka dhidi yake.
Rugemalira amekuwa huru dhidi ya kesi hiyo baada ya kukaa mahabusu kwa muda mrefu tangu alipofikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Juni 19, 2017 akikabiliwa na kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 27/2027 yenye mashtaka 12.
Mapema leo katika Mahakama ya Hakim Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam, upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa serikali, Grace Mwanga umedai mahakani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wa Mahakama hiyo kuwa kesi dhidi ya Rugemalira iliitwa Mahakamani kwa ajili ya kutajwa lakini DPP amewasilisha hati ya kuiondoa kesi hiyo (Nolle Prosequ) chini ya kifungu cha sheria cha 91 (1) cha mwenendo wa makosa ya jinai.
Licha ya hayo Juni 2017, Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa nchini Tanzania TAKUKURU iliwafikisha Mahakamani Mkurugenzi wa Kampuni ya Kufua Umeme (IPTL), Herbinder Seth na Rugemalira kwa makosa sita ya uhujumu uchumi ikiwemo kosa la kuisababishia serikali hasara.
Aidha katika shtaka jingine, Washtakiwa wote, walidaiwa kuwa kati ya Novemba 28/29, 2011 na Januari 23,2014 Makao Makuu ya Benki ya Stanbic Kinondoni na Benki ya Mkombozi tawi St Joseph zote za Dar es salaam, kwa ulaghai, walijipatia kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh. 309, 461,300,158.27.
Iliendelea kudaiwa kuwa katika shtaka la kusababisha hasara, washtakiwa hao walidaiwa kwamba mnamo Novemba 29, 2013 katika Benki ya Stanbic tawi la kati Kinondoni kwa vitendo vyao waliisababishia Serikali hasara ya Dola za Marekani 22, 198, 544.60 na fedha za Kitanzania Sh 309,461,300,158.27.
Post a Comment