Dar es Salaam, leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi kwa
kumteua Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dk. Yamungu Kayandabila kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).
Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Jaffar Haniu imesema Rais Samia pia amemteua Dk. Naomi Bakunzi Katunzi kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa kipindi kingine cha miaka mitatu na kuongeza kuwa Uteuzi huo ulianza juzi, Septemba 14, 2021.
Post a Comment