Featured

    Featured Posts

SHAKA: SERIKALI YA RAIS SAMIA ITAENDELEA KUTOA ELIMU BILA MALIPO

Nachingwea, Lindi

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesisitiza kwamba Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kutoa elimu bila malipo. 


Amesema, Serikali itaendelea kufanya hivyo ikiwa ni utekelezaji wa waraka wa elimu namba 6 wa mwaka 2015 na Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.


Shaka amesema hayo wakati akikagua Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Nachingwea iliyopo katika Kata ya Chiumbati mkoani Lindi, akiwa katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo na Sekretarieti, iliyoanzia mkoani humo, jana.


 Amese, hakuna ahadi yoyote iliyotolewa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025  ikiwemo mpango wa elimu bila malipo na utatuzi wa changamoto za sekta ya elimu nchini ambayo haitakelezwa.


"Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kugharamaia elimu bila malipo. Ikiwa ni utekelezaji wa waraka wa elimu namba 6 wa mwaka 2015 na ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025", Amesema Shaka.


Aliwataka wananchi wapuuze taarifa zozote za upotoshaji ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya watu zikidai serikali itasitisha mpango huo wa kugharamia elimu bila malipo.


Shaka alisema, kutokana na dhamira ya dhati, Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Samia imeendelea kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ikiwemo kuajiri walimu takribani 6,949.


Amesema mbali na kuajiri idadi hiyo ya Walimu, katika Bajeti ya 2021/22 imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 125 za kukamilisha maboma 10,000 nchi nzima yote hayi ikiwa ni utekelezaji wa ibara ya 80 ya ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.


Shaka amewapongeza wananchi wa Kata hiyo ya Chiumbati, Kijiji cha Chiumbati shuleni, kwa kutoa eneo la ujenzi wa shule hiyo, kujitolea nguvu kazi na hata kuchangia ujenzi katika hatua za awali kabla ya serikali kuwaunga mkono kuendeleza ujenzi huo.


Wananchi wa eneo hilo nao wamemshukuru Rais Samia katika kuipa kipaumbele elimu na kufanikisha hatua za ujenzi wa shule hiyo ya wavulana  ambayo wamesema ilikuwa ni hitaji lao la muda mrefu.


Akizungumzia Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika mwakani,  Shaka amewataka wananchi kujitokeza kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa hiyo. 


Alifafanua kuwa serikali inatekeleza zoezi hilo kwa kuwa taarifa zake zina umuhimu mkubwa katika kuisaidia kupanga rasilimali zake katika maendeleo ya nchi na watu wake hivyo ni muhimu kila mmoja kujitokeza kulishiriki.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, akipaka rangi wakati akikagua Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Nachingwea Kata ya Chiumbati mkoani Lindi, leo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana