Featured

    Featured Posts

MBUNGE AGEUKA KULI, WANANCHI WASHANGILIA NA KUMPONGEZA

Mbunge wa Ludewa, Joseph Kamonga akisaidia kubeba viroba vya mahindi
katika kituo cha ununuzi wa  mahindi Mlangali, Ludewa.
Msimamizi wa Ununuzi wa Mahindi wa NFRA, Hosea Mathias akiongea kwa simu na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.

Kamonga akiwa amezungukwa na wakulima alipokuwa akiongea kwa simu na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kutafuta ufumbuzi wa serikali kununua mahindi wilayani humo.
Kamonga akiangalia mahindi katika ghala  la NFRA, Mlangali Ludewa.




Na Richard Mwaikenda, Dodoma
BAADHI ya Wakulima na Wabeba mizigo  kwa malipo  maarufu kama Makuli, wameshangilia na kumpongeza  walipostaajabu kumuona Mbunge wa jimbo lao la Ludewa, Joseph Kamonga akiungana nao kubeba viroba vya mahindi kilo 50.


Tukio hilo lililowastaajabisha wakulima na Makuli hao limetokea  katika kijiji cha Mlangali kilipo kituo cha kununulia mahindi cha  Wakala wa Taifa wa Uhifadhi wa Chakula (NFRA) wilayani Ludewa, Njombe.

Wengi wao hawakuamini alipowaambia kuwa anataka awasaidie kusomba viroba hivyo, ambapo alitega mabega yake na kubebeshwa kiloba cha mahindi cha kilo 50 ambacho alikibeba toka nje hadi ndani ya ghala na kupandisha ngazi hadi juu vilipokuwa vinapangwa.

Kuona hivyo, walimshangilia huku wengine wakimpongeza kwa uthubutu na ujasiri alioufanya kuwasaidia kubeba mzigo huo tofauti na viongozi wengine.

"Yes, huyu ndiyo mbunge tunayemtaka, anajichanganya kwa kila jambo kuwasaidia wananchi wake, hatutaki wabunge bishoo," alisikika mmoja wa Makuli huku akiungwa mkono na wenzie.

"Hongera sana mbunge wetu, tumekuona ukisaidia kubeba viroba,  hatukuamini lakini tumeshuhudia kwa macho yetu, Mungu azidi kukulinda uendelee kuongoza jimbo letu," Calitus Haule alimpongeza huku wengine wakiendelea kumpigia makofi.

Baada ya hapo, Kamonga aliendelea na jitihada zake za kutatua changamoto ya kuwatafutia wakulima soko la tani 16,000 za ziada za mahindi zilizokwama wilayani humo baada ya NRFA kununua tani 1000 tu.

Akiwa amezungukwa na wakulima,  aliamua kumpigia simu Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe na kumueleza changamoto hiyo huku nao wakisikiliza, ambapo Bashe aliagiza simu hiyo apewe msimamizi wa kituo, Hosea Mathias  na kumtaka wafanye tathmini ya tani halisi za ziada zilizopo wilayani humo li serikali ipate ufumbuzi wa haraka kuzinunua.

Kusikia hivyo, zililipuka nderemo na vifijo huku wakiendelea kumpongeza Mbunge Kamonga kwa jitihada zake za kuwapigania. 

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza/kuona  yalizojiri katika tukio hilo....
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
 Mhariri Blog Ya Taifa Ya CCM
 0754264203
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana