Featured

    Featured Posts

RAIS SAMIA, TURUFU MUHIMU KATIKA SIASA ZA KIMATAIFA

 

 Na Dk Juma Mohammed

Kwa mara ya kwanza, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atahutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa akiwa Rais wa kwanza mwanamke wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Septemba 23 mwaka huu, Rais Samia atahutubia Baraza Kuu linalowakutanisha Viongozi 193  wa nchi wanachama wa UN katika mkutano wa 76 wa Baraza hilo katika Viunga vya Jiji la New York, Marekani.  

Mkutano huu sio tu ni muhimu kwa nchi wanachama ikiwemo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,lakini pia ni fursa ya kipekee kwa Rais wetu kukutana na viongozi wenzake kutoka Mataifa mbalimbali wanaohudhuria mkutano huo.

Katika mkutano wa Baraza Kuu, Palestina na Vatican City (Holy See) hawa ni wajumbe wasiokuwa wanachama wa Umoja wa Mataifa wakiwa watazamaji wa kudumu wa Baraza Kuu la UN.

Ulimwemngu wa leo si wa kujifungia ndani, lazima utoke ujumuike na wenzako na kwa kupitia mikutano ya aina hii, bila shaka nyota ya Rais Samia katika anga la Kimataifa inazidi kung'aa, Tunaona fahari kubwa kwa Rais wetu kuzungumza na Dunia kupitia mkutano huu muhimu ambapo Tanzania itaueleza Ulimwengu.

Rais Samia anabaki kuwa turufu muhimu katika siasa za Kimataifa sio tu za hapa kwetu, bali katika Afrika tukiwathibitishia Walimwengu kuwa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia isiyokumbatia mfumo dume kama tunavyoona katika baadhi ya mataifa.

Safari ya Rais Samia kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa inanikumbusha kisa kimoja kilichosimuliwa na Sheikh Bassaleh ambae alisimuliwa na rafiki yake juu ya mkasa uliomkumba.

Alinieleza safari moja alijiwa na matapeli lakini waliojifanya ni watu wa dini. Walimwomba awasaidie kufanikisha maulid wanayotaka kusoma kwa kuwasaidia kuwapa vifaa vya pilau.  

Walimwambia wao wamekamilisha kila kitu, lakini bado wanahitaji mchele, mafuta ya kula na nyama tu,  

Yule rafiki yangu akawajibu inaonekana ninyi hamjafanikisha lolote maana huo mchele, mafuta na nyama mnayotaka nikupeni ndiyo hiyo pilau yenyewe.   

Ninyi mmefanikisha nini? Basi wao wakajibu tumekamilisha asilimia kubwa ya vitu tumenunu kuni, vitunguu, viazi, mdarasini, bizari nyembamba, chumvi n.k.   

Ni kweli kwa idadi ya vitu wao wamekusanya vitu vingi; lakini vitu vyote hivyo viki changanywa pamoja haviwezi kupika pilau.   

Pilau hasa ni huo mchele, mafuta na nyama. Kama huna vifaa hivyo vitatu, hata uwe na vifaa vingine vingi sana, hutaweza kupika pilau.   

Kisa hichi nakinasibisha na haja ya kukuza uhusiano wa kimataifa.
Kukaa ndani peke yake hakukufanyi kuweza kusonga mbele, unahitaji kutoka nje kuungana na viongozi wenzako wa kimataifa katika kutafutia ufumbuzi changamoto zinazokabili dunia.

Katika Ulimwemngu unaoendelea kwa kasi, ni jambo muhimu sana kwa kiongozi wa nchi kushiriki katika siasa za Kimataifa yeye mwenyewe maana siku zote kuagiza ni kufyekeza

Anaposimama Mkuu wa Nchi kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa inakuwa ni tofauti unapotuma mwakilishi katika mkutano huo.

 Tukumbuke kuwa katika Viunga vya New York, mbali ya Wakuu wa Nchi na Serikali, pia kunakuwa na Wakuu wa Mashirika mbalimbali ya Kimataifa ambao kukutana nao kuna faida nytingi katika maendeleo ya nchi yetu.

Rais Samia, akiwa Mwanadiplomasia nambari moja Tanzania, atakuwa kioo na mwangaza katika kuijenga na kuimarisha sera yetu ya mambo ya nje kupitia mkutano huo na mikutano mengine ya kimataifa.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana