Viongozi kutoka Mkoa wa Dar es Salaam wakiingia ukumbini kwa ngoma ya segere ya kumtoa mwali wakati wa tamasha hilo.
Na Richard Mwaikenda, Moshi
Mchanganyiko wa ngoma za utamaduni za makabila mbalimbali zililipamba Tamasha la Utamaduni katika Kambi ya Mafunzo elekezi kwa viongozi wapya wa Chama Cha Tanzania Girl Guides (TGGA), mjini Moshi.
Ngoma hizo zilichezwa kiumahiri usiku na viongozi kutoka mikoa 20 ya Tanzania Bara na Visiwani pamoja na vijana wa YES kutoka nchi za Zambia na Uganda. Kila mkoa walijitahidi kucheza kiushindani kwa lengo la kuwashawishi majaji kuibuka washindi hivyo kuibua vifijo, nderemo na vigeregere hasa kutoka na baadhi yao kucheza huku wakiwa wamevalia nguo za kiume. Wawakilishi wawili wa YES kutoka Zambia wakitia fora kwa kucheza kiustadi ngoma ya kwao na kufanya Ukumbi kurindima KWA kuwapigia makofi. Ngoma hizo zilikuwa zinaratibiwa kiustadi na DJ machachari Valentina Gonza huku shindano hilo likiongozwa na mshereheshaji MC Mamyto kutoka Mkoa wa Pwani. Tamasha hilo lilifanyika sambamba na maonesho ya bidhaa za asili ya mikoa hiyo. Baada mashindano hayo kumalizika, Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi aliwapongeza wote kwa kushiriki vyema katika tamasha hilo na hatimaye alitangaza mshindi wa kwanza hadi wa tano ambao ni: Zanzibar, Lindi, Tanga, Arusha na Mara.
Mkoa wa Dar es Salaam na ngoma yao ya segere |
Majaji wa Tamasha hilo.
Mkoa wa Singida na ngoma ya Mawindi.
Mkoa wa Kilimajaro
Mkoa wa Kilimanjaro na ngoma ya kumtoa mwali.
Mkoa wa Lindi washindi wa pili.
Mkoa wa Mara washindi wa Tano
Mkoa wa Mtwara
Mkoa wa Ruvuma na ngoma ya Lizombe
Mkoa wa Tabora
Mkoa wa Tanga na ngoma ya Mdumange.
Mkoa wa Dodoma
Vijana wa Yes wakisakata ngoma
YES kutoka Zambia wakicheza ngoma ya kwao.
Zanzibar washindi wa kwanza
Bi Sauda wa Zanzibar.
Zanzibar wakiingia ukumbini huku wakiwa na miamvuli
Mdau, nakuomba uendelee kuona kupitia kwenye clip hii ya video yaliyojiri kwenye tamasha hilo.....Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
Post a Comment