Na CCM Blog, Chalinze
RAIS mstaafu Dk. Jakaya Kikwete amesema Rais Samia Suluhu Hassan analeta matumaini kwa Watanzania kwa manufaa ya nchi ya leo na kesho na kwamba nchi inakwenda vizuri kutokana Serikali anayoiongoza kuonekana kutatua changamoto kwenye sekta mbalimbali Nchini.
Amesema miongoni mwa Sekta ambayo Serikali ya Rais Samia inaonekana kuendelea kutatua changamoto zake ni Sekta ya Afya ambapo Serikali hiyo imeendelea kuiimarisha ikiwemo kutambua umuhimu wa kuongeza wigo wa huduma za dharula
Dk. Kikwete aliyasema hayo wakati wa kutembelea eneo litakalojengwa Mradi wa jengo la matibabu ya dharula katika Hospital ya Wilaya ya Chalinze iliyopo Msoga mkoa wa Pwani, ambao umefadhiliwa na Mfuko wa Uwezeshaji Huduma za Afya wa kampuni ya ABBOTT ya nchini Marekani, kwa gharama ya Bilioni 1.2.
Alifafanua kuwa msaada uliotolewa kwa ajili ya jengo hilo ni wa Sh. Bilioni 1.2 ikiwa ni sawa na Dola 500,004 za Marekani na tayari walishashiriki kusaidia masuala mbalimbali nchini ikiwemo kutoa vifaa milioni moja vya kupimia Virusi vya Ukiwmi.
“Sijafanikisha peke yangu hili, mie niliweka msukumo, lakini namshukuru sana Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, wakati huo Dorothy Gwajima ambae ndie ali 'push' suala hili, Niseme tu namshukuru sana ”alisema Dk. Kikwete.
Aidha ameiomba Serikali, itoe mafunzo kwa madaktari na watumishi wa afya kuhusiana na masuala ya dharula ili miradi kama hiyo itakapokamilika kusiwepo na changamoto ya ukosefu wa wataalamu wa dharula na kuiomba jamii na watumishi wa umma waendelee kumuunga mkono Rais Samia, kwa kuchapa kazi na kuwataka vijana kujituma ili kujiepusha na kuwa mzigo katika jamii.
Kwa upande wake Naibu waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Godwin Molleli alisema Serikali imetenga tayari imetenga fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha huduma za afya nchini ikiwemo kiasi cha sh. Bilioni 187 kwa ajili ya kujenga Kiwanda Cha chanjo za UVIKO19, zitakazozalishwa hapa nchini, Sh. Bilioni moja kwa ajili ya kununua magari ya wagonjwa 150 ambayo yatasambazwa nchini ambapo kati ya hayo Jimbo la Chalinze litapatiwa gari moja kati ya hayo.
Morell alisema Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete aliomba Sh. Milioni 418 kwa ajili ya umaliziaji wa majengo ya ujenzi wa hospital ya wilaya na serikali imeridhia kutoa fedha hizo kwa awamu
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mbunge huyo Ridhiwan Kikwete alisema juhudi zinaendelea kumaliza baadhi ya majengo katika hospital ya wilaya Chalinze, ambayo imetolewa bilioni moja katika ujenzi wa majengo matano ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 83.
Mwakilishi kutoka ABBOTT, Frenk Kanza alisema, Kampuni hiyo inajishughulisha kutengeneza bidhaa za maabara Duniani ila kwa msaada huu umetokana na fedha kutoka mfuko wa uwezeshaji wa masuala ya afya na kuishukuru Serikali kwa, msamaha wa Kodi ya kiasi cha Dola 40,000 za Marekani, suala ambalo lilichangia kuchelewesha Mradi na kukwama kwa muda wa miezi miwili na kuongeza kuwa ujenzi wa mradi huo September mwakani.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Pwani, Abubakari Kunenge ambaye alihudhuria hafla hiyo, alisema mkoa huo una maeneo mengi yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji hivyo itapendeza kiwanda Cha chanjo ya Uviko 19 kikajengwa mkoani Pwani.
Alieleza, pia mkoa umeshapokea Bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa vituo vinne vya afya vinne vitakavyojengwa kwenye tarafa, fedha ambayo imetokana tozo za miamala ya simu na kuongeza kuwa watasimamia Mradi huu kwani unakwenda kutatua changamoto za kiafya na wanashukuru inakwenda kufungua mkoa wa Pwani kimaendeleo.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akichambua nyaraka zake wakati wa Makabidhiano rasmi ya nyaraka za mradi wa Jengo la Huduma za dharura katika Hospitali ya Wilaya ya Chalinze, Msoga mkoa wa Pwani.Kushoto ni Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete na Naibu Waziri Molleli Naibu waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Godwin Molleli akikabidhi nyaraka hizo kwa Mkuu wa mkoa wa Pwani Aboubakar Kunenge wakati wa hafla hiyo. Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akitoa maelezo kuhusu mradi huo kwa Naibu waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Godwin Molleli Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akitoa maelezo kwa
Naibu waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Godwin Molleli wakati wa kutembelea mradi huo
Post a Comment