Featured

    Featured Posts

MWAKITINYA ATOA ELIMU YA UPIGAJI KURA , AKIMWOMBEA KURA CHEREHANI WA CCM, USHETU

Mjumbe wa halmashauri kuu ya (CCM) Musa Mwakitinya (MNEC) ametoa elimu ya upigaji kura kwa wananchi (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Sabasabini.


Wazee wa kimila wa kata ya Mpunze wakimwekea mikono mgombea ubunge wa jimbo la Ushetu,Emmanuel Cherehani ikiwa ni ishara ya kumwombea dua ili awezekushinda katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Oktoba tisa mwaka huu.
Baaadhi ya wananchi waliojitokeza katika mikutano ya hadhara ya kampeni za uchaguzi jimbo la Ushetu.


Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Santile Kirumba akimwombea kura mgombe ubunge wa jimbo hilo,Emmanuel Cherehani,kushoto ni Idd Kassim mbunge wa jimbo la msalala na kushoto ni Lucy Mayenga mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga.

 Wananchi wa kata ya Mpunze wakimwagia maji ya baraka mgombea ubunge wa jimbo la Ushetu,Emmanuel Cherehani ikiwa ni ishara ya kumbariki katika safari yake ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.


SALVATORY NTANDU

USHETU.

3/10/2021

Ili kuhakikisha chama cha mapinduzi (CCM) kinapata ushindi katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Ushetu, mjumbe wa halmashauri kuu ya (CCM) Musa Mwakitinya (MNEC) ametoa elimu ya upigaji kura kwa wananchi katika mikutano mbalimbali ya hadhara ya kumnadi na kumwombea kura mgombea wa chama hicho, Emmanuel Cherehani ifikapo Oktoba tisa mwaka huu.

Alisema kuwa CCM imejipanga kuhakikisha inapata ushindi katika uchaguzi huo mdogo,ili kuendelea kuwahudumia wananchi ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo maji,afya,elimu na miundombinu ya barabara ambayo baadhi yake imeanza kutekelezwa.

“Niwaombe wananchi wa jimbo hili kwanza mkahakiki taarifa zenu katika katika daftari la kupigia kura katika vituo mlivyojiandikishia ili ikifika siku ya uchaguzi,ukipata karatasi ya kupigia kura wewe angalia mgombea wa (CCM) Emmanuel Cherehani,”alisema Mwakitinya.

Alifafanua kuwa chama pekee kitakachowavusha wananchi wa jimbo hilo ni CCM pekee wasiwapigie kura wapiga debe wasiokuwa na ilani ya uchaguzi inayotekelezwa wanye uchu wa madaraka na badala yake wamchague mgombea wa chama hicho ambaye anafaa kuwa mbunge wa jimbo hilo.

“Wapo wapiga debe wanapita vijijini kuomba kura kwenu,kwanza waulizeni wanaomba kura ili wakafanye kazi na nani?,kwani viongozi wote waliopo madarakani ni wa CCM kuanzi ngazi ya kitongoji hadi taifa,”alisema Mwakitinya.

Nae Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama, Thomasi Myonga alisema kuwa maendeleo ya kweli yanapatikana ndani ya chama hicho pekee na wasidanganyike na ahadi zisizotekelezeka zinazoahidiwa na upinzani ambao hauna hoja zenye tija.

“Msichanganye punda na ng’ombe mnapotaka kulima shamba hawataendana,Ushetu ninayoijua mimi ni yakijani kuanzia shina,matawi,kata,na majimbo,mnachotakiwa ni kumchagua Cherehani ili akaendeleze yaliyoanzishwa na mtangulizi wake Elias Kwandikwa,”alisema Myonga.

Kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo hilo, Emmanuel Cherehani alisema kuwa endapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha anatatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi kama vile umeme na maji.

“Nimepita katika maeneo mengi bado wananachi wanakabiliwa na tatizo la maji,kupitia chama change tutahakikisha maji ya ziwa viktoria yanafika ushetu na maeneo ambayo hayana umeme yatawekewa kupitia mradi wa REA II awamu ya tatu,”alisema Cherehani.

Sambamba na hilo Cherehani alisema akipata ridhaa ya kuliongoza jimbo hilo atahakikisha katika uongozi wake wananchi wanapata huduma bora za afya ikiwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa mabomba ya zahanati na vituo vya afya vilivyoanzishwa kwa nguvu za wananchi.

Uchaguzi mdogo wa jimbo la Ushetu unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Elias John Kwandikwa na Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa kufariki dunia mwaka huu.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana